Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Mamba Sweya leo amewaita wafanyabiashara, wakandarasi na mafundi ujenzi wanaoidai Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Katika kikao hicho Ndugu. Sweya amewataka kila mtu anayeidai Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa alete nyaraka zote zinazothibitisha uhalali wa madai yake ili kuweza kuhakikiwa na hivyo baadae kuanza kulipwa. Katika kikao hicho wadai wote pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wamehudhuria katika kikao hicho.
Hata hivyo katika kikao hicho Mkurugenzi aliiteua Kamati Maalum itakayofanya kazi ya kupitia, kukagua, kuchambua na kuandika taarifa sahihi ya madai ya kila mmoja ili Halmasahuri iweze kulipa madeni hayo. Katika Kamati hiyo ameteuliwa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Ndug. Godfrey Ayako, Mweka Hazina Ndug. Emmanuel Abraham, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Ndug. Joseph J. Manyanga, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi Ndug. George Mwakajinga na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi Ndug. Rashidi A. Rashid. Kamati hiyo imetangazwa mbele ya wadai hao.
Akielezea Ndug. Sweya amesema "nimefikia uamuzi huu wa kuunda Kamati Maalum ya Kuhakiki madai yenu kwasababu madeni mengine ni ya muda mrefu, nyaraka za madai hazipatikani na watumishi waliokuwa wanafahamu madeni hayo hawapo".
Kwa upande wa wadai, wakiongozwa na Mfanyabiashara maarufu wa vifaa vya Ujenzi Ndug. Marandu, ambaye ni Mwenyekiti wa wafanyabiashara wameridhia kwa pamoja kuwa madeni yao yahakikiwe ili yaweze kulipwa kwa kupeleka nyaraka za madai yao mbele ye Kamati iliyoundwa na Mkurugenzi Mtendaji.
Wadai wa Halmashauri na Wakuu wa Idara wakiwa katika kikao cha pamoja kujadili utaratibu utakaotumika kuhakiki madaeni (Kushoto) Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndug. Khamlo Njovu.
Aidha katika kikao hicho wamekubaliana kuwa zoezi hilo la kuhakiki madai ya wafanyabiashara yaanze kufanyaka kuanzia leo na Kamati imesema iko tayari kwa kazi hiyo kuanzia sasa.
***Mwisho***
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.