Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na baadhi ya Waku wa Idara wenye miradi kukagua na kujiridhisha kuwa hatua zilizofikiwa katika maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo inafaa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2018. Katika ziara yake Mkuu wa Wilaya amepongeza hatua nzuri iliyofikiwa na kukosoa kasoro chache zilizojitokeza katika miradi hiyo ili zirekebishwe. Kamati za ujenzi pamoja na Wakuu wa Idara wenye Miradi wamepokea kasoro hizo na wamehaidi kuzishughulikia karoso hizo ili miradi iwe ya kiwango kinachoridhisha na kama ilivyo katika mchoro. Pia ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 30 Julai 2018 Wilaya ya Mpwapwa inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2018. Wilaya ya Mpwapwa itaupokea Mwenge wa Uhuru kimkoa ukitokea Mkoa wa Morogoro Wilayani Kilosa.
Baadhi ya Miradi iliyotembelewa na imefika katika hatua nzuri ni kama ifuatavyo:-
1. Shule ya Msingi ya Franco Badian iliyopo kata ya Lumuma.
Shule hii ni ya Awali na Msingi na inamilikiwa na kanisa Katoliki ambapo wanafunzi wanaosoma ni wa kutwa. Kipindi cha ukaguzi wa awali shule hii haikuwa na vibao vya madarasa, kibao cha shule, masinki ya vyoo yalikuwa machafu na jengo la utwala halikuwepo. Kwa sasa vibao vyote tayari vimetengenezwa bado kubandika katika milango ya madarasa. Pia jengo la utawala lipo katika hatua ya usawa wa madirisha na linatarajiwa kumalizika mwezi Septemba 2018.
Jengo la Utawala la Shule ya Franco Badiani limefikia usawa wa madirisha na ujenzi unaendelea. (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akikagua vibao vya kuonyesha madarasa katika Shule ya Franco Badiani . (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Mafulu akikagua vyoo vya Shule ya Franco Badiani . (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
2. Mradi wa Kituo cha Afya Pwaga
Katika kituo hiki hatua ya awali ilikuwa imefikia katika lenta, kwa sasa imefikia hatua ya kuezekwa bati, kufuma mbao kwa ajili ya kuweka ceiling board (blandering) pamoja na kupachika madirisha ya nondo. Pia ujenzi unaendelea.
Jengo la Kituo cha Afya cha Pwaga kikiwa kitika hatua ya kuezekwa bati na kupachikwa madirisha (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Jengo la Kituo cha Afya cha Pwaga kikiwa katika hatua ya blandering (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
3. Mradi wa Barabara ya Kidenge - Lufu.
Katika ukaguzi wa awali barabara hii ilikuwa katika hatua ya kuwekwa vifusi vya udongo, kwa sasa imemwagwa changarawe na bado ipo katika ujenzi.
Barabara ya Kidenge - Lufu ikiwa katika kiwango cha changarawe (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
4. Kituo cha Wanayama Kazi Kibakwe.
Katika ukaguzi wa awali kituo hiki kilikuwa hakina mazao ya kutosha ya kuweza kuonyesha siku ya mwenge, ila kwa sasa kumepandwa mahindi, kabichi, nyanya maji, mboga za majani na pilipili hoho
ambazo zinaendelea vizuri. Vile vile kuna shamba la vitunguu ambavyo vimepandwa hivi karibuni na havijashika vizuri chini.
Hosteli za kituo cha Wanyamakazi Kibakwe hutumika wakulima wanakuja kufanya mafunzo (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (wa kwanza kulia) akipata maelezo kwenye shamba darasa la kituo cha Wanyamakazi Kibakwe (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
5. Shamba la Korosho katika Kitongoji cha Mbuyuni
Shamba hili lina ukubwa wa ekari 5 na lilipandwa miche ya mikorosho 125 kati ya hiyo 10 tu ilikufa na kubaki 115 tu ikiwa na afya nzuri. Katika ukukaguzi wa awali ilionyesha miche inadhoofika kwa kushambuliliwa na wadudu baada ya kupuliziwa dawa na kwa sasa inaendelea vizuri. Kazi iliyobaki ni kutengeneza barabara ya kuingilia na kupalilia shamba hilo ambapo mmiliki wa shamba hilo amesema atapalilia.
Moja ya Mche wa mkorosho katika shamba la mikorosho katika Kitongoji cha Mbuyuni (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
6. Kiwanda cha Kukamua Mafuta ya Alizeti, Kusaga nafaka (Mahindi)
Kiwanda hicho kipo Mpwapwa eneo la Ilolo, kinanunua alizeti na mahindi toka kwa wakulima. Kinakamua alizeti kupata mafuta na kuyauza kwa ajilili ya matumizi ndani na nje ya Mpwapwa. Pia kinasaga nafaka ya mahindi ili kupata unga ambao unawekwa katika mifuko maalum tayari kwa kuuzwa nje na ndani ya Mpwapwa. Kiwanda hicho kijulikana kama Akyoo Mills, wanakamua mafuta ya alizeti na Kutengeneza Sangito Super Sembe.
Kiwanda cha Kukamua Alizeti na Kusaga nafaka (Mahindi) (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Kiwanda cha Kukamua Alizeti na Kusaga nafaka (Mahindi) na hizi ni baadhi ya mashine (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha Akyoo Mills (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.