Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh Dkt Sophia Mfaume Kizigo ameyafunga rasmi mafunzo ya ya jeshi la akiba Julai 31,2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Gulwe.
Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 1,2025 yakiwa jumla ya Wanafunzi 205,miongoni mwao wanaume 105 na wanawake 30,wakati wa mafunzo hayo wanafunzi 104 walishindwa kuendelea na mafunzo kutokana na sababa mbali mbali ikiwemo changamoto za kiafya,uvivu,nidhamu mbovu na kupotoshwa na watu wenye uelewa mdogo na suala la ulinzi na usalama pamoja na utoro sugu, hivyo kupelekea wanafunzi 101 ndio waliohitimu mafunzo hayo ,ikiwa wanaume 85 na wanawake 17,mafunzo yaliyotolewa kwa muda wa mienzi minne katika kata ya Gulwe.
Hata hivyo,JP Masanja amesema dhumuni kubwa la mafunzo hayo ni kuwaandaa Wananchi kuwa tayari katika suala la ulinzi na usalama wa Taifa letu na kutegemea ushiriki mzuri bila uoga katika suala la Ulinzi,vilevile mafunzo hayo yametolewa kwa nadharia na vitendo kwa kila Mtanzania mzalendo aliyejitokeza kwa hiyari yake mwenye umri unaoruhusiwa kushiriki.
Naye Mhe.Dkt Kizigo amewataka wahitimu hao kuendeleze nidhamu na heshima waliyokuwa nayo na kuepukana na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa.
Pia amewataka wananchi kwa ujumla kulinda afya zao kwa kila kitu.
"Tunategemea askari awe na nidham,hatutegemei mwende mtaani muwe vijeba mnatukana watu tutakufuta kwenye uaskari"
"Sisi sote tulinde afya zetu kwa kila kitu,tujupende jamani tupende Afya zetu"Amesema Dkt Kizigo
Dkt kizigo amewapongeza wazazi na wakufunzi wa wahitimu hao kwa jitihada kubwa walizozifanya kufanikisha mafunzo hayo na kufunga rasmi mafunzo ya jeshi la hakiba yaliyofanyia katika kata ya Gulwe.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.