Wagonjwa wametakiwa kuwa na utaratibu wa kwenda kwa wataalam wa afya kwa ajili ya matibabu ya uhakika na sio kwenda kwa Waganga wa Kienyeji au kununua dawa kwenye maduka ya dawa pasipo na fuata maelekezo ya wataalam.
Hayo yamesisitizwa Septemba 29,2025 na Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Mpwapwa Dr Stanley Mlay wakati akifungua rasmi huduma za Mkoba katika Kituo cha Afya Ipera.
Hata hivyo amesema,katika kuunga mkono kampeni ya Mhe Rais, Dr Samia Suluhu Hassan ya kusogeza huduma za Mama na Ma Dakatari bingwa hadi ngazi za afya ya Msingi,Halmashaùri ya Wilaya ya Mpwapwa imeanzisha utaratibu wa utoaji wa huduma hizo katika maeneo ya kata mbali mbali ambazo zina zahanati pamoja na vituo vya Afya.
Utaratibu wa huduma hizo unajulikana kwa jina la huduma za mkoba za kliniki kwa ajili ya magonjwa sugu pamoja na upimaji wa afya ya mama wajawazito na watoto wachanga ikiwa na lengo la kusogeza huduma za matibabu karibu na Wananchi kutokana na uwepo wa idadi kubwa watu wenye uhitaji wa huduma hizo
Aidha, huduma ambazo zinatolewa ni pamoja na magonjwa ya ndani ikiwemo magonjwa sugu, magonjwa ya mama wajawazito pamoja na watoto, huduma za uchunguzi kwa kutumia sonographia, upasuaji pamoja na huduma za macho kwa siku mbili kwa kila kituo.
Zoezi hili linaendeshwa na kauli mbiu isemayo '
'Tuzingatie taratibu za matibabu ya kitaalam kwa ustawi ya afya zetu" ambapo kwa Kata ya Ipera,Malolo na Chipogoro litafanyika hadi Octoba 3,2025.






Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.