Mjumbe kamati kuu ya CCM Taifa Ndug.Donald Mejitii amewataka Watumishi wa Serikali kutoa huduma bora kwa jamii zinazoendana na ubora wa majengo yaliyojengwa na Serikali ya awamu ya sita
Ameyasema hayo Julai 16,2024 wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma ya kukagua miradi na kujionea utekelezaji wa ilani ya Chama.
“Mama Samia amefanya kazi kubwa sana ya kujenga majengo ya Afya na vifaa vyake na Wananchi wanafurahiya huduma zinazotolewa lakini bado hatujapata muunganiko mzuri wa watumishi wa afya na majengo hayo”
“Mgomjwa amefika kupata matibabu saa 12 asubuhi ,mtumishi anafika saaa 4 hiyo sio huduma”Amesama Mejitii
Aidha Ndg.Mejitiin amewasihi wananchi wa Wilaya hiyo hususan kata ya Gulwe,kuhakikisha wanawapeleka watoto wao Shule ili kuwaanda wataalam wa mambo mbalimbali hapo baadae na kuondokana na ujinga.
Katika ziara yake hiyo amekagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa kikundi cha ushonaji nguo kilichopo Kazania,mradi wa bwawa la Msagali liliopo Mbugani,mradi wa barabara kutoka Kongwa_Mpwapwa na kutoka Mpwapwa_Kibakwe,ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Chazungwa na Zahanati ya kijiji cha Chiseyu.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.