Katika kuunga mkono Dhamira ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka wa fedha 206/2017 ili kuongeza kasi ya kufikia lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025, Diwani wa kata Ipera Wilayani Mpwapwa Mhe. Festo Myuguye amewekeza katika shughuli za Kijasilia mali zenye mrengo wa kuongeza thamani ya bidhaa za mazao yanayolimwa wilayani hapa. Mhe Festo anasema kuwa amebaini fursa katika eneo lake lenye uzalishaji mkubwa wakaranga kwa kutumia mashine za kubangua karanga ili kuweza kuongeza thamani ya zao hilo ambapo awali karanga zenye maganda zilikuwa zikiuzwa kwa gunia na sasa karanga zilizobanguliwa zitauzwa kwa kilo. Mbali na faida watakayoipata wakulima kwa kuuza mazao yao kwa bei nzuri, pia Mhe Diwani anasema ameamua kuwekeza kwenye shughuli halali za kuongeza kipato.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.