Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wameitaka Halmashauri yao kuunga mkono jitihada ambazo wananchi wamekuwa makizifanya katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo ili kuweza kusogeza huduma karibu kwa Wananchi. Hayo yameafikiwa katika kikao kazi cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Tarehe 28.04.2017 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Akiwasilisha Hoja katika Baraza hilo Mhe Mangile Said Maulid, Diwani wa Kata ya Malolo alisema kuwa wananchi wamekuwa wakihangaika kutembea umbali mrefu katika kutafuta huduma ya matibabu, ni vema kama Halmashauri itaunga Mkono jitihada za wananchi ambao wamekwisha anza kujenga zahanati ambapo ujenzi upo katika hatua ya lenta katika Kata ya Malolo. Hoja hii iliungwa mkono na madiwani wote ambao wameitaka Halmashauri kutoa kipaumbele katika kumalizia miradi viporo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.