Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wametoa Motisha kwa Watumishi wanaofanya kazi kwa kujituma ikiwa ni mkakati wa kujenga hamasa na kuwatia moyo ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Wanufaika wa Mpango huo ni pamoja na Ndugu Dorice Dario, Mwanasheria wa Halmashauri ambaye amesaidia Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuweza kushinda kesi mbali mbali suala ambalo halijawahi tokea. Akikabidhi zawadi kiasi cha Tsh 100,000.00 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe Donati Nghwenzi alitoa wito kwa watumishi wote kutekeleza majukumu yao kwa kujituma huku wakitanguliza Uzalendo. Mwananshheria huyu alipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi Mtendaji, Wajumbe wa Kamati ya Fedha Pamoja na Madiwani wote kwa ujumla. Utoaji wa zawadi umefanyika katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Tarehe 29.04.2017 ( Katika picha ni Ndugu Dorice Dario, Mwanasheria wa Halmashauri aliyepewa Motisha)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.