Wadau wa Maji wameadhimisha Kilele cha wiki ya maji wilayani Mpwapwa mnamo tarehe 23.03.2017. Maadhimisho hayo katika ngazi ya wilaya yamefanyika katika kata ya Chitemo ambapo wadau walikutana katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa wilaya pamoja na vijiji. Akitoa maneno ya nasaha, mgeni rasmi katika mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bw.Emmanuel Saro, amewataka wananchi kutunza miradi ya maji hususani miundo mbinu iliyojengwa na serikali kwa gharama kubwa.Ametoa wito huo huku akisisitiza kuwa utunzaji miundo mbinu huo ni muhimu ili miradi iliyopo iweze kudumu na kutatua changamoto ya adha ya maji kwa wananchi.
Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Maji katika kata ya Chitemo (Picha kwa hisani ya Erick Urassa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.