Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa
Uongozi wa Mradi wa LIC (Local Investment Climate Project) leo umewakutanisha Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashaurii ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donalth S. Nghwenzi pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya hiyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Katika kikao hicho kilichokuwa na mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na mwakilishi toka LIC ambaye pia ni msimamizi wa Miradi yote ya LIC katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Donald, ameleza lengo kuu la kuwakutanisha Madiwani na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni kuwaleta pamoja katika kusimamia miradi ya LIC katika maeneo yao.
Waheshimiwa madiwani na wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakisiliza kwa makini tathmini ya mradi wa LIC katika kutekereza miradi iliyopo Mpwapwa, kwenye Ukumbi wa Halmashauri (Picha Na: Shaibu Masasi - Afisa TEHAMA)
Donald anasema "Wataala wa Halmashauri wa Wilaya ya Mpwapwa wanatoa ujuzi wa kitaalam katika miradi, wakati madiwani mnatoa hamasa na ushawishi kwa wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi pamoja kushimamia uhalali wa matumizi ya fedha kulingana na thamani halisi ya mradi". Hivyo ametoa wito wa madiwani na wakuu wa idara au wataalam kukaa pamoja kujadili na kuufahamu mradi kabla ya kwenda kutekeleza.
Meza kuu ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donalth S. Nghwenzi (katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndug. Maria Leshalu (Kushoto) na Makamu Mwenyekiti Mhe. George Fuime (Kulia) wakisiliza tathmini ya mradi wa LIC katika Ukumbi wa Halmashauri (Picha Na: Shaibu Masasi - Afisa TEHAMA)
Vile vile Donald, ameeleza kuwa LIC imefadhiri miradi mingi yenye fedha nyingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikiwemo miradi ya kufunga mtandao kiambo katika jengo la Halmashauri , kununua Mashine za Kielektroniki za Kukusanyia mapato (POS) 12, kununua Kompyuta 10, printa 4, barcode reader mashine 2, kujenga kituo cha biashara na kuweka miundombinu yote, kufadhiri kituo cha wanyamakazi Kibakwe, Ujenzi wa Mfereji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kata ya Lumuma, kufadhiri uendeshaji na vikao vya baraza la biashara na ujenzi wa Mnada wa Ilolo kata ya Mpwapwa Mjini. Hii ni baadhi tu ya miradi ambayo LIC imeifadhiri na inakarikbisha maandiko zaidi ya miradi mbalimbali.
Waheshimiwa madiwani na wakuu wa idara wa Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa wakisiliza kwa makini tathmini ya mradi wa LIC katika kutekereza miradi iliyopo Mpwapwa, kwenye Ukumbi wa Halmashauri (Picha Na: Shaibu Masasi - Afisa TEHAMA)
LIC imetoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutekeleza na kusimamia miradi yote ya LIC vizuri maana kuna maeneo mengine wameshindwa kusimamia na kusababisha fedha kuondolewa kupelekwa mahali kwingine kwenye uhutaji, lakini kwa Mpwapwa haijawahi kutokea hili. Ndug. Donald ameeleza.
Kwa maelezo zaidi pakua nyaraka Hizi (Bofya hapa chini)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.