LGTI yaanza kujenga uwezo kwa WEO,VEO,MEO kuhusu O&OD yenye Mwelekeo wa Tabianchi na Usawa wa Kijinsia Wilaya Mpwapwa
Novemba, 12 2025, Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) kwa kushirikiana na UNCDF kupitia mpango wa LoCAL, wamezindua mafunzo ya siku tatu kwa Watendaji wa Kata (WEOs), Watendaji wa Vijiji (VEOs) na Watendaji wa Mitaa (MEOs) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Mafunzo haya ni mwendelezo wa awamu ya awali iliyotolewa kwa Wawezeshaji wa Kata (WFs) na Kikosi Kazi cha Halmashauri cha O&OD (CTF) katika Wilaya za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa. Awamu hii inalenga kuimarisha uwezo wa viongozi wa ngazi za chini kuingiza masuala ya mabadiliko ya tabianchi na usawa wa kijinsia katika mipango shirikishi ya maendeleo kupitia mbinu ya Improved O&OD.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni Kuwajengea watendaji hao uwezo wa vitendo katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia mipango ya maendeleo inayozingatia mabadiliko ya tabianchi, usawa wa kijinsia, na ushirikishwaji wa makundi yote ya jamii hasa wanawake, vijana, na watu wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Katika ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo, viongozi wa Halmashauri ya Mpwapwa wamepongeza juhudi za LGTI na UNCDF, wakibainisha kuwa:
“Improved O&OD ni mfumo rasmi wa serikali kwa kupanga maendeleo kwa njia shirikishi. Kuongezewa kwake kipengele cha mabadiliko ya tabianchi kunakifanya kuwa nyenzo madhubuti katika kusaidia utekelezaji wa mipango na bajeti zinazohimili athari za tabianchi kulingana na mahitaji halisi ya jamii."
Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza ushirikiano kati ya WEOs, VEOs, MEOs, na Wawezeshaji wa Kata (WFs) ambao ndiyo wawezeshaji wa moja kwa moja wa jamii katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo zinazohimili mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway, ambao unapitia UNCDF kufadhili utekelezaji wa mpango wa LoCAL – Local Climate Adaptive Living Facility nchini Tanzania.
Kwa upande wa Mpwapwa, halmashauri inajiandaa kupokea ruzuku za LoCAL ambazo zitaelekezwa kwenye miradi ya kuongeza ustahimilivu wa jamii, ikiwemo miradi ya maji, kilimo na mifugo kwa kuzingatia vipaumbele vitakavyotokana na mchakato wa Improved .





Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.