Mwenge wa Uhuru 2018 umewasili leo tarehe 30 Julai 2018 wilayani Mpwapwa ukitokea wilaya ya Kilosa Mkoani Mororgoro. Ambapo kwa mwaka huu Mkoa wa Dodoma umepokea Mwenge huo wa Uhuru wilaya ya Mpwapwa katika kata ya Lumuma. Katika mapokezi hayo viongozi mbalimbali walihudhuria na baadhi yao ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Stephen Kebwe, aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndug. Rehema Madenge na katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro, wakuu wa wilaya zote za Dodoma na Morogoro, makatibu tawala wote wa wilaya za Morogoro na Dodoma, wakuu wa jeshi la polisi wa mikoa na wiilaya ya Morogoro na Dodoma, na viongozi wengine walioambatana na hao, pamoja na wananchi kwa ujumla.
Mwenge uliwasili majira ya saa 2.30 asubuhi hivi ukiwa chini ya kiongozi wa mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho akiambatana na makamanda wengine wa kitaifa. Mwenge huo umepokelewa na Katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma na Kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Jabir Shekimweri kwa ajili ya kuukimbiza katika wilaya ya Mpwapwa.
Mwenge wa Uhuru 2018 umetembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi sita yenye jumla ya Tsh 2,171,782,580.00 ikiwepo miradi ya Elimu, Kilimo, Barabara, Afya na Kiwanda. Katika miradi yote sita hakuna hata mradi mmoja uliokataliwa na mkimbiza mwenge wa kitaifa. Miradi yote ilipokelewa vizuri, ila mradi wa kituo cha afya Pwaga mkimbiza mwenge kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho ameupokea na kuweka jiwe la msingi lakini ametoa maelekezo ya kuboresha mradi huo ambapo mkuu wa wilaya ya Mpwapwa amekubali kuyatakeleza maelekezo hayo.
Pia wilaya ya Mpwapwa kupitia michango ya mwenge ambayo imechangwa na kuvuka lengo, imenunua pikipiki aina ya boxer kama zawadi kwa jeshi la polis ili kupamba na uharifu pamoja na madawa ya kulevya, imetengeneza DVD 6 za matukio yote ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 na kuwakabidhi wakimbiza mwenge, pamoja na kutoa zawadi mbalimbali.
Aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndug. Rehema Madenge (mwenye kilemba kichwani) akipokea Mwenge wa Uhuru 2018 kutoka kwa katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro mara tu baada ya kuwasili Mkoani Dodoma , Wilaya ya Mpwapwa, Kata ya Lumuma. (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mwenge wa Uhuru 2018 umetembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzidua Miradi sita kama ifuatavyo:-
1. Shule ya Msingi ya Franco Badian iliyopo kata ya Lumuma.
Shule hii ni ya Awali na Msingi na inamilikiwa na kanisa Katoliki ambapo wanafunzi wanaosoma ni wa kutwa. Shule hii imejengwa chini ya ufadhiri na imegharimu kiasi cha Tsh. 674,500,000.00.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2018 kitaifa Ndug. Charles Francis Kabeho ameusifu sana mradi huo wa shule na ametoa wito kwa wadau wengine kuwekeza katika Elimu kwa kuwa serikali imeamua kufuta ada mashuleni ili jukumu la mzazi kwa mwanafunzi liwe ni kumnunulia mahitaji ya muhimu na chakula. Pia ametoa wito wa wazazi kuchangia chakula kwa watoto wao ili waweze kula wakiwa shuleni, ila ametahadharisha kuwa michango hiyo ikusanywe na kamati maalum itakayoundwa na wazai wenyewe.
Baada kupata taarifa ya kina ya mradi huo mkimbiza mwenge kitaifa amekagua na kujiridhisha, na hivyo kukubali kuuzindua mradi huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho akizindua shule ya Franco Badian kata ya Lumuma Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho (watatu kulia) akitoa ujumbe wa mwenge katika shule ya Msingi Franco Badian kata ya Lumuma Wilayani Mpwapwa. Akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (wapili kulia). ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
2. Mradi wa Shamba la Vitunguu Lumuma.
kiongo wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 ametembelea mradi wa kilimo cha vitunguu katika shamba la kikundi cha wakulima kata ya Lumuma. Akisoma taarifa ya mradi mmoja wa wanakikundi cha shamba hilo alitaja mafanikio wanayoyapata kupitia mradi huo ni kupata fedha ya kujikimu kimaisha, ujuzi wa namna ya kutumia nyenzo za kilimo katika kufanikisha kilimo bora ili kujipatia kipato cha kutosha.
Pia ametaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na kutopatikana wa pembejeo za kilimo kwa wakati, kushuka na kupanga kwa bei ya zao la vitunguu na kutokuwa na soko la uhakika.
Baada ya kusomewa taarifa fupi, kiongozi wa mbio za mwenge amekagua mradi huo na kuwasifu wanakikundi kuwekeza katika kilimo cha zao la biashara. Pia amekabidhi cheti kwa kikundi cha wakulima hao.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho (wapili kulia) akisomewa taarifa fupi ya mradi wa shamba la vitunguu kata ya Lumuma Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho akikagua mradi wa shamba la vitunguu kata ya Lumuma Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho akikabidhi cheti kwa wakulima wa kikundi cha mradi wa shamba la vitunguu kata ya Lumuma Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
3. Mradi wa Kituo cha Afya Pwaga
Kituo cha Afya Pwaga kipo kata ya Pwaga wilaya ya Mpwapwa, kituo hiki ni cha serikali na kipo katika hatuo ya umaliziaji wa ujenzi huo ambapo majengo yote yamekamilika na yapo katika hatuoa ya mwisho ya umaliziaji. Majengo hayao ni kama vile jengo la wagonjwa wa nje (OPD), wodi ya kinamama, wadi ya wanaume, wodi ya watoto, jengo la kuhifadhi maiti, na chumba cha upasuaji. Kituo hiki mapaka kukamilika kwake kitagharimu Tsh. 502,250,000.00 ambapo fedha toka serikali kuu ni Tsh. 500,000,000.00 na fedha toka katika nguvu za wananchi ni Tsh. 2,250,000.00.
Baada ya kusomewa taarifa fupi ya kituo, mkimbiza mwenge wa uhuru 2018 amekagua na kutoa maelekezo kuwa matofali yote yaliyotengewa katika njia zinazounganisha jengo moja na lingine yabomolewe kwa kuwa matofauli hayo yapo chini ya kiwango. Ila katika majengo yote amesifu kuwa yamejengwa vizuri na kwa kiwango kinachoridhisha kwa kutumia Local Fundi. Aidha mkuu wa wilaya ya Mpwapwa amepokea maelekezo ya mkimbiza mwenge huyo na kuhaidi kuyafanyia kazi na kuboresha zaidi.
Baada ya kukagua, kuhoji na kupata maelezo ya kina juu ya mradi huu Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2018 amekubali kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho akikagua matofali yaliyojengewa njia zinazounganisha jengo moja na lingine katika mradi wa Kituo cha Afya Pwaga kata ya Pwaga Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Said Mawji akisoma taarifa fupi mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndug. Charles Francis Kabeho katika mradi wa Kituo cha Afya Pwaga kata ya Pwaga Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
4. Ujenzi wa barabara ya Kidenge - Lufu
Barabara ya kidenge ilianza kujengwa mwaka 2017 ambapo Mwenge wa Uhuru 2017 uliweka jiwe la msingi. Mwaka huu 2018 mwenge wa Uhuru umezindua barabara hii ikiwa imekamilika kwa 90% ila kazi ya kumalizia ikiendelea. Barabara hii itagharimu kiasi cha Tsh 764,470,080.00 mpaka kukamilika kwake.
Baada ya kusomewa taarifa fupi, Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2018 amekubali kuzingua barabara hii.
Mwenge wa Uhuru 2018 ukiwa umewasili katika barabara ya Kidenge - Lufu, Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Wananchi wakiwa katika barabara ya Kidenge - Lufu wakiushangilia Mwenge wa Uhuru 2018 , Wilayani Mpwapwa. ( Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
5. Shamba la Korosho la Mkulima Shabani Mlindoko
Shamba hili lilianza kupandwa miche ya mikorosho mwezi Februari 2018 na lina ukubwa wa ekari 5, miche hai ikiwa 115 na miche 10 ilikufa, hivyo miche iliyopandwa ilikuwa 125. Miche hiyo imepandwa kitaalam kwa kuzingatia ushauri wa maafisa kilimo ambapo imepandwa kwa umbali wa mita 12 kutoka shina hadi shina. Shamba hili mpaka sasa limegharimu kiasi cha Tsh 562,500.00, fedha zote zikiwa ni za mkulima mwenyewe. Pia Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imemsaidia mkulima huyo miche ya mikorosho pamoja na dawa ya kuua wadudu waharibifu wa korosho. Vile vile inatoa ushauri wa kilimo kwa wakulima wote ikwemo wakulima wa zao jipya la kororsho.
Moja ya mikorosho iliyopo katika shamba la mkulima Shabani Mlindoko lilotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2018 katika kitongoji cha Mbuyuni Wilayani Mpwapwa (Picha. Na: Shaibu. J. Masasi, Afisa TEHAMA -Mpwapwa)
6. Kiwanda cha Kukamua Alizeti na Kusaga Nafaka (Mahindi)
Kiwanda hiki kinajulikana kwa jina la Akyoo Mills na kinajishughulisha na kukamua mafuta ya alizeti na kusaga nafaka za mahindi ili kupata unga wa sembe. Kiwanda hiki kimegharimu jumla ya Tsh. 230,000,000.00 mpaka kukamilika. Kwa sasa kiwanda kimeshaanza uzalishaji na kuuza bidhaa zake nje na ndani ya mkoa wa Dodoma. Pia kiwanda kinanunua alizeti na mahindi kutoka kwa wakulima hivyo wakulima wamepata soko la mazao yao kupitia uwepo kwa kiwanda hiki.
Baada ya kusomewa taarifa, Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2018 kitaifa amekagua na kuhoji maswali machache kisha akazindua kiwanda cha Akyoo Mills. Pia ametoa wito kwa wananchi kwa kikundi au mtu mmoja mmoja kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati hasa katika viwanda vinavyotumia mazao ya kilimo kwa kuwa malighafi yanapatikana.
Akyoo Mills Kiwanda cha Kukamua Alizeti na Kusaga nafaka (Mahindi) (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akikagua kiwanda cha Akyoo Mills cha Kukamua Alizeti na Kusaga nafaka (Mahindi) (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Unga wa sembe unaozalishwa na kiwanda cha Akyoo Mills unajulikana kwa jina la Sangito Super Sembe (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.