Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Mohamed O. Mchengerwa(Mb) Leo Mei 23, 2025 amefungua Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Ukumbi wa Mikutano DodomaJiji ulipo Mji wa Serikali Mtumba.
Katika Kikao Kazi hicho Mhe Mchengerwa amewataka Maafisa Habari Nchini kutoa taarifa sahihi ya yale yanaoyoendelea kwenye maeneo yao.
" Ninyi ni nguzo ya maamuzi ya kuwalisha watanzania ya kile kinachoendelea katika maeneo yenu" Amesema Mhe Mchengerwa (Mb)
Pamoja na hayo Mhe Mchengerwa amewataka Maafisa Habari kuweka Uzalendo mbele katika kuisemea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao.
Kikao hicho kitaendelea kwa siku mbili ambapo Maafisa Habari kote Nchini wamekutana kuendelea kubadilishana uzoefu namna bora ya kuzitangaza kazi za Serikali katika maeneo yao.
Miongoni mwa Halmashauri zilizoshiriki Kikao Kazi hicho kutoka Dodoma ni pamoja na Mpwapwa,Chemba,Kongwa,Chamwino,Dodoma Jiji,Bahi,Kondoa tc na Kondoa Dc.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.