Wanafunzi nane wa Shule ya Msingi Mbori katika Wilaya ya Mpwapwa wamefunikwa na kifusi cha mchanga baada ya kutumwa na mwalimu wao kwenda kuchota mchanga katika kingo za mto Mbori kwa ajili ya ujenzi wa choo katika shule hiyo. Kwa mujibu wa masuhuda wanafunzi hao walikwenda kutochamchanga katika eneo hilo mto bila kuwa na usimamizi wa mwalimu na hivyo kupelekea kuchota mchanga katika kingo za mto na kusababisha kufundikwa na kifusi baada ya kingo ya mto kubomoka.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya wazazi wenye hasira waliokusanyika katika Jengo la Zahanati ya Mbori, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat Paul Maganga amesema "Sisi kama viongozi wa Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi tumepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa, hivyo naomba kutoa taarifa rasmi kuwa wanafunzi waliofariki ni watatu ambayo ni Rehema Alex ni binti wa darasa la nne, wapili ni Daudi Enock Macheha wa darasa la tano na watatu ni Ezra Lucas Hamis ni mwanafunzi wa darasa la Sita. Pia kuna wanafunzi watano wamejeruhiwa ambao ni wa kwanza Arafa Athumani wa darasa la nne, wapili ni Nelly David Amosi wa darasa la Sita, watatu ni Wiston Ezekiel wa darasa la nne, wanne ni Yunis Musa Sango wa darasa la nne, nawatano ni Mwajuma Michael wa darasa la tano ". Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa, kwa hiyo wanafunzi watatu hatupo nao tena na hawa wanafunzi watano majerehi kwa taarifa nilizonazo wanne wako hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa na wanaelea vizuri ila mmoja yupo hapa katika Zahanati ya Mbori amechunguzwa hajapatashida yoyote na hivyo amepumzishwa hapa. Ila majeruhi wote wanaendelea vizuri na wataruhusiwa leo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat P. Maganga Akitoa taarifa ya Vifo na Majeruhi Katika Tukio la Wanafunzi kufunikwa na Kifusi cha Mchanga Katika Mto Mbori.
Aidha mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Serikali amesema "kuna vyombo vya dora ambavyo vimepewa dhamana ya kukamata, kuchunguza na kupeleka mahakamani, hivyo jambo hili litachunguzwa na kuwachukulia hatua wahusika, sawa watoto wamefariki kuna masawali ya kujiuliza Je, nani aliwatuma?, Je, ilikuwa ni wakati wa darasani?; hili jambo lazima tujiridhishe nalo, kazi ya mwanafunzi ni kwenda kusoma". Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuwa watulivu kwa kuwa Serikali inalichunguza jambo hili na wahusika watafikishwa mahakamani.
Vile vile Mkuu wa Wilaya Ametoa maelekezo manne muhimu;- 1. Kazi za kusomba mchanga, maji, kokoto na matofali kwa wanafunzi zimepigwa marufuku, kazi za maenedeleo ziachwe kwa wazazi, 2. Mazizshi ya wanafunzi waliofariki yatafanywa na Serikali kwa kuandaa majeneza na sisi viongozi tutakwenda kuwazika watoto waliofariki, 3. Kulikuwa na suala la vijana wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mbori kufanya mitihani ya majaribio ya mkoa, huo mtihani nimeuhairisha kutoka kesho na utafanyika tarehe 02/08/2021 kwa kuwa wanafunzi hao watakuwa na majonzi na hawataweza kufanya mitihani hii, 4. Nimesikitika Kitendo cha wananchi kwenda kuharibu mali za shule kwa sababu ya tukio hili, mmeharibu shule, mmeboa milango, na kutoboa mabati nawashauri suala hili lisirudiwe tena muwe wavumilivu kwa sababu ukifanya fujo utachukuliwa hatua kama muarifu mwingine.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat P. Maganga Pamoja na Viongozi wengine wa Wilayaa Akiwa katika Eneo la Tukio la ambapo Wanafunzi walifunikwa na Kifusi cha Mchanga Katika Mto Mbori.
Naye shuhuda wa tukio hilo Bwana. Issa Makangu ameseme "Ilikuwa asubuhi nikiwahi shambani kwangu kwa ajili ya kumwagilia, niliwapita wanafunzi waliokuwa wakizoa mchanga, ghafla nikiwa shambani kwangu nilisikiaa kishindo kikubwa na wanafunzi wakiwa wanapiga kelele, haraka nikawahi kuona ni nini kilikua kimetokea. Nilikuta wanafunzi wamefukiwa na mchanga baadhi waliweza kujitoa ila wengine walishindwa hivyo nikaanza kuwatoa, nilifanikiwa kuwatoa wanafunzi saba na ndipo akatokea mama mmoja aliyekua katika majukumu yake ya kawaida tukawa tunasaidiana, kadri tulivyokua tunautoa mchanga na kuchimba chini tulisikia sauti ya mtoto ikilalamika kwa sauti ya chini sana na tukafanikiwa kumtoa japokuwa hakuwa na nguvu kabisa. Kelele za wanafunzi zilizidi na ndipo raia wakazid kuongezeka, kwa pamoja tukafanikiwa kuwatoa watoto wengine sita (6), tuliwauliza watoto kama wanafahamu idadi yao ila hawakuwa wanafahamu kwa hiyo tulizidi kuchimba chini ili kuangalia kama tunaweza kuwaona wengine tulifanya hivyo mpaka tulipojiridhisha kuwa hakukuwa na mtoto aliyebakia."
Wananchi wa Kijiji cha Mbori wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat P. Maganga Akitoa taarifa ya Vifo na Majeruhi Katika Tukio la Wanafunzi kufunikwa na Kifusi cha Mchanga Katika Mto Mbori.
Mwisho, Wananchi wamemuomba Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Maganga kufunga Eneo hilo ili lisitumike tena kuchota mchanga wa kuwa ni hatarishi. Nawe Mkuu wa Wilaya ameridhia ombi hilo na eneo litafungwa rasmi na ameagiza kufungwe utepe na kiwekwe kibao chenye maandishi yanayoonyesha hakuna mtu yeyeyote kufanya shughuli yoyote katika eneo hili.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.