“Uhuru na Kazi “, “Uhuru na Maendeleo”, “Uhuru na Umoja”, “Kilimo cha Kufa na Kupona”...... Tanzania ya Viwanda
Tangu kupatikana kwa uhuru nchini mwaka 1961 serikali iliweka msisitizo mkubwa kwa jamii kujitegemea na kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kikamilifu katika kazi za kujenga taifa. Ikumbukwe kuwa Kampeni mbalimbali zenye ujumbe maalum wa kuhimiza shughuli za kujitegemea na uelimishaji zilitumika mfano: “Uhuru na Kazi “, “Uhuru na Maendeleo”, “Uhuru na Umoja”, “Kilimo cha Kufa na Kupona”. Katika kuleta ufanisi wa juhudi hizo viongozi wakuu wa serikali na mashirika mbalimbali walishiriki kwa vitendo katika kazi za maendeleo ya kijamii na kiuchumi wakiwa kama vielelezo vya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu.
Siku za hivi karibuni imeonyesha kuwa jamii imesahau majukumu yao na kuachia serikali hali inayosababisha maendeleo ya wananchi kurudi nyuma. Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuamsha na kukuza ari ya wananchi kufanya kazi kwa bidii. Halmashauri ya wilaya Mpwapwa imepanga siku Maalum ya Kazi za Maendeleo ili kuinua ari ya wananchi kujitolea na kushiriki katika kazi za maendeleo katika kila kijiji iwe ni JUMATANO ya kila wiki. Siku hiyo itatumika na wananchi katika vijiji vyao kupanga shughuli kwa pamoja na kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Afisa maendeleo (W) Khamlo Njovu anatanabaisha kuwa uwepo wa siku maalumu ya kufanya kazi una umuhimu Umuhimu wa kuanzishwa kwa siku Maalum ya kuinua ari ya jamii kumezingatia mahitaji mbalimbali ya kikatiba, Kisera, Sheria ya Nguvu Kazi ya mwaka 1983, hali halisi ya ongezeko la mahitaji ya jamii, kasi ya ukuaji wa uchumi na Mipango mbalimbali ya maendeleo ya Taifa. Utekelezaji wa siku hii unatarajiwa kuleta tija katika mambo yafuatayo:
A : KIJAMII
B : KIUCHUMI
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.