(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Khamlo Njovu ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Paul Sweya, amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa. Katika mafunzo haya wadau mbalimbali wa LISHE Endelevu wamehudhuria kama vile Jukwaa la Utu wa Mtoto, Action Against Anger, Save the Children, Taasisi ya Chakula na lishe, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma, Diloitte, Wakuu wa Idara, Viongozi wa dini, taasisi binafsi zinazojihusisha na mashuala ya LISHE.
Madhumini ya mafunzo haya ni kuwapitisha wajumbe wa Kamati ya LISHE Wilaya katika Mpango Mkakati wa Wa Taifa ambao umetaja kila majukumu ya wadau wa LISHE toka ngazi ya Kitaifa, Wizara, Mikoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji mpaka kwa jamii. Mpango Mkakati huo umeeleza masuala mengi ya lishe ikiwemo jinsi ya kuwashirikisha wadau wengine katika masuala ya lishe ambao ni muhimu.
Wajumbe wa kamati ya LISHE Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Wadau wa LISHE wakiwa katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa wakifuatilia mafunzo ya LISHE
Aidha mtoa mada ameutambulisha Mpango Mkakati wa Taifa wenye agenda na shughuli mbalimbali kuanzia ngazi ya wizara hadi katika ngazi ya jamii. Pia ameongeza kuwa katika Mpango Mkakati kila mdau anategemea mdau mwingine, mfano: wadau wa kilimo wanawategemea wadau wa viwanda na sekta ya maji, hivyo double duty interaction ina maana kuwa katika masuala ya LISHE wadau mbalimbali wanapaswa kuhusishwa.
Pia Mpango mkakati umeainisha bayana namna ya kufanya ufuatiliaji na tathmini katika ukekelezaji wa shughuli za LISHE zilizofanywa na kuwashrikisha wadau mbalimbali wa lishe kama wazalishaji wa vyakula, vinywaji, na chumvi ili kuweza kuwahamasisha kuweka virutubisho muhimu katika bidhaa wanazozizalisha lengo likiwa ni kuiwezesha jamii kupata virutubisho hivyo kupitia bidhaa wanazozitengeneza na kuziuza kwa jamii.
Vilevile kamati ya LISHE imefundishwa namna ya kufahamu Utapiamlo mkali ambao husababishwa na mtu kutopata chakula cha kutosha na kisichokuwa na virutubisho kama vitamini, madini chumvi, protein na virutubisho vingine.
Aidha Mpango Mkakati wa Taifa huu umefuata mabadiliko ya jamii kama kupata chakula bora, afya bora, ukosefu wa rasilimali, kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, ini, figo na shinikizo la juu la damu, hivyo tunatazamia kuwa watoto, wanawake, vijana na wanaume watakuwa na afya bora ya kuweza kufanyakazi na kuzalisha mali.
Wajumbe wa kamati ya LISHE Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Wadau wa LISHE wakiwa katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa wakifuatilia mafunzo ya LISHE
Mpango huu wa Mkakati wa Taifa umetaja matumizi ya vyoo bora na kutumia kanuni za afya vizuri ili kuepukana na kupata magnjwa ya mlipuko kama kipindupindu na hivyo wananchi kuwa na afya imara.
Mwisho wajumbe wa Kamati ya LISHE Wilaya wamegawiwa Tool Kit na Kitini cha Masuala ya LISHE kama vitendea kazi katika majukumu yao ya kila siku ya LISHE. Pia Mwenyekiti wa Mafunzo hayo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amewashukuru wote waliotoa mafunzo haya na ameaidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa niaba ya wajumbe wote wa kamati ya LISHE Wilaya ya Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.