Kaimu Mkuu wa Wilaya Ndg Obert Mwalyego ambae ni Afisa Tarafa wa Kata ya Mpwapwa ,Novemba 13,2025 amefanya ziara ya kukagua miradi ya Afya iliyojengwa na SRWSS PROGRAM katika kituo Cha Afya Mbori na Zahanati ya Inzovu.
Katika kata ya Kimaghai ametembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Inzovu ambayo imegharimu kiasi cha shilingi 60,170,00 kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa P4R kwa ajili ujenzi wa mnara wa tank la maji na ununuzi wa lita 10,000,kitakasa mikono,kichomea taka,shimo la kondo la nyuma la mama baada ya kujifungua,choo cha watumishi na choo cha wateja pamoja na kufanya maboresho ya chumba cha kujifungua,Miradi imekamilika kwa asilimia 100.









Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.