Jamii yahimizwa kuwajibika kuendeleza kuchanja mbwa na paka wao kila baada ya mwaka chanjo hiyo inapotolewa.
Hayo yamebainishwa Leo Septemba 28,2025 na Ndg Obert Mwalyego kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mhe Dkt Sophia Mfaume kizigo wakti wa maadhimisho ya siku ya kichwaa cha Mbwa Dunia,ambapo kwa Wilaya ya Mpwapwa yameeadhimishwa Jumba la Maendeleo Mjini.
Halikadhalika,ameitaka jamii kutambua ugonjwa wa kichaa cha Mbwa ni hatari na wanapaswa kuchukua tahadhari mapema na pindi inapotokea mtu ameng'atwa na mbwa hatua za haraka zichukuliwe
Pia amewasisitiza viongozi wa dini wazidi kutoa elimu kwa waumini wao pindi mtu akipata tatizo hilo kukimbilia Hospital na sio kwenda Polisi.
"Lazima mtambue kwamba ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni hatari
"Kila mmoja wetu ahakikishe anachukua hatua za haraka akiumwa na mbwa na sio kukimbilia Polisi"Amesema Ndg Mwalyego
Aidha,Mganga Mkuu wa hamshauri Dr Stanley Mlay ameelezea sababu za ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na kusema,kichaa cha mbwa kinasababishwa na virusi ambavyo huwa vinapatikana kwa wanyama kama mbwa na paka na pindi vikizalishwa kwa vingi bila kupatiwa chanjo na kutokea kumuuma mtu ugonjwa huo hutokea.
Hata hivyo,amesema dalili mbalimbali hujitokeza kwa mtu aliyepata kichaa cha mbwa ikiwemo kujiskia homa,kutoa mate na misuli kukakamaa na hata kubweka kama mbwa.
Nae, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na UvuviDr Emanuel Lymo amesema Mbwa 2500 wanatarajiwa kuchanja wakiwemo na Paka,vilevile amewashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha zoezi hilo ikiwemo Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Wizara ya Afya,INADES,TAWESO na kadhalika.
Chanjo ya kichaa cha Mbwa hutolewa kwa mwaka mara moja na pindi ikitokea mtu ameumwa na mbwa ambae ana kichaa inaushauriwa kusafisha sehemu iliyopata jeraha kwa maji tiririka na sabuni lakini pia kukimbilia kitoa cha Afya kwa haraka.





Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.