Taasisi ya INADES wamefanikiwa kuunda jukwaa la kumtunza na kumlinda mnyama punda kwa leng kwa
Lengo la kuhakikisha jamii inapata elimu na uwelewa wa namna ya kumtunza mnyama punda.
Engineer Patrick Lameck kutoka Taasisi ya INADES formation,Tanzania yenye makao Makuu yake Dodoma,Septemba 25,2025 katika ofisi za Kilimo Mpwapwa ameendesha warsha na kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusiana na kumtunza mnyama punda.
Halikadhalika,ameendesha zoezi la kuundwa rasmi jukwaa la wadau ambalo kwa kawaida huundwa na wadau kuanzia 20 hadi 30 kwa muda wote watakaokuwepo litatumika kumtunza mnyama punda,pia ameelezea majukumu ya jukwaa hilo ikiwemo kutambua wadau husika kwa ajili ya kutatua changamoto zitakazojitokeza katika jamii inayomlinda mnyama huyo.
Aidha,Mnyama Punda ameelezwa kuwa ni mnyama ambaye anastahili kutunza nankuimarisha afya na huduma zake kama wanyama wengine kwa kuzingatia misingi ya wanyama wengine chini ya wastani wa wanyama Na.19 ya mwaka 2008.




Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.