Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imeagizwa kuandaa Mwongozo wa kushughulikia Malalamiko mbali mbali ya wananchi ili iweze kutambua changamoto mbali mbali za wananchi na kuzishughulikia kikamilifu. Hayo yamesisitizwa na Mratibu wa Utawala wa Utumishi wa Umma- IKULU, Francis Mang'ira katika Kikao kazi cha Kukumbushana Wajibu na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Leo tarehe 12.09.2017 katika Ukumbi wa Halmashauri. Mang'ira Amesema kuwa Pamoja na kuwa na Mwongozo wa jumla wa kushughulikia Malalamiko, kila Halmashauri inapaswa kuandaa Mwongozo wake wa kushughulikia Malalamiko utakaoendana na Mazingira yake halisi.
Sanjari na hilo ametaka kuwepo na Bango linaloelekeza zilipo ofisi za Dawati la Malalamiko na ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano baina ya Dawati la Malalamiko, Wakuu wa Idara pamoja na Kamati za Uadilifu. Katika kupunguza Malalamiko Watumishi wa Umma wameaswa kuwajibika ipasavyo na msisitizo mkubwa uwe katika kufanyika kwa Mikutano na vikao vya Kisheria vya Watumishi Vijiji na Halmashauri. Vile vile Watumishi wameaswa kuyatambua majukumu yao na kuyatekeleza kikamilifu kwa kuzingatia Sheria, Taratibu , Kanuni Miongozo na Nyaraka mbali mbali kama alivyosisitiza Mratibu Msaidizi wa Utawala wa Utumishi wa Umma- IKULU, Abdallah Said Mwongane.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.