Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa yazindua mpango wa taifa wa utoaji wa chajo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wanye umri wa miaka 14 kama maelekezo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yanavyo hitaji. Chanjo hiyo imezinduliwa leo na kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Apolonia Temu katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa leo tarehe 30/05/2018. Katika uzinduzi huo wananchi wote wamehudhuria pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Mpwapwa Mjini.
Wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya ambayo inatekeleza zoezi la kitaifa la uzinduzi wa chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa kizazi kwa mabinti wenye umri wa miaka 14, Uzinduzi huu umefanyika katika Hospitali ya wilaya ambapo walengwa ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za hapa mjini kama zifuatavyo: sekondari ya mwanakianga, Mazae, Mount Igovu, Ihala, Qeen Ester na Vighawe. Pamoja na uzinduzi huu zoezi hili linaendelea katika vituo vyote vya kutolea huduma vya Afya vikiwemo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Binafsi.
Wanafunzi wakisubiri taratibu za kupimwa na kupewa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi (Picha. Alutha Kimbe, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
katika hotuba yake Mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Mpwapwa amesema "Saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na vitu vingi ikiwemo kuanza kujamiana katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuwa na ndoa za mitala, kuzaa watoto wengi, na uvutaji wa sigara". Pia ameongeza kuwa dalili za saratani ya mlango wa kizazi mara nyingi hujitokeza ikiwa imeshasambaa mwilini. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za saratani mfano; kutokwa damu ya hedhi bila mpangilio, kutokwa damu baada ya kujamiiana, maumivu ya mgongo, miguu na/au kiuno, kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa au kokosa hamu ya kula, kutokwa uchafu wa rangi ya kahawia au wenye damu kwenye uke, maumivu ya miguu au kuvimba.
Wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao ni wanafunzi akipatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi wilayani Mpwapwa
Pia mgeni rasmi ameongeza kuwa dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kupatwa na fistula, na uvimbe wa tezi. Lengo hasa la kuanzisha chanjo hii ni kukinga mabinti wetu kutokana na madhara makubwa yanayoweza kuwapata ambayo husababisha vifo vingi kwa wanawake, na hivyo kuboresha afya za jamii ya wanawake Watanzania kwa ujumla. Uanzishwaji wa chanjo hii utahusisha pia Mkoa wetu.Walengwa wa chanjo hii kwa mwaka huu wa 2018 ni wasichana wote wanaotimiza miaka 14, ambao kwa wilaya yetu ya Mpwapwa tunatarajia kuchanja mabinti wapatao 4046.Katika uzinduzi huu tutaanza na shule zote za Sekondari zilizopo hapa mjini ambapo uzinduzi wake unafanyikia katika Hospitali ya wilaya. Kutokana na ratiba za shaule zoezi hili linatarajiwa kukamilika kablaya kufungwa kwa shule.Chanjo hii hutolewa kwa dose mbili yaani (dose 1wakati wowote dose ya pili baada ya miezi 6) Ndugu Wananchi/Wanafunzi.
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mpwapwa wakiwa katika uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Mwisho mgeni rasmi ametoa wito wa wananchi wote kwa ujumla kuwa na muamko wa kuwahamasisha wa watoto wao wakike wenye umri wa miaka 14 kupata kinga na waliozidi umri huu kuweza kupima saratani ya mlango wa kizazi. Ili kujilinda na saratani ya mlango wa kizazi, njia ya kwanza ni kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi, kutokufanya ngono katika umri mdogo, kuepuka kubeba mimba katika umri mdogo.
Napenda pia niwataarifu mkakati utakaotumika katika utoaji wa chanjo hii. Kutokana na uzoefu uliopatikana wakati wa majaribio ya utoaji wa chanjo hii Mkoani Kilimanjaro, chanjo hii itatolewa katika utaratibu wa kawaida katika vituo vyetu vya kutolea huduma za chanjo, baadhi ya shule zitakazochaguliwa, na baadhi ya maeneo katika jamii ambapo zitatolewa kwa njia za huduma za mkoba.Huduma hizi zitatolewa bila malipo katika vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali na binafi.Chanjo hii imethibitishwa kuwa ni salama na haina madhara yoyote. Wizara yetu kwa kushirikiana na wadau tumejipanga vizuri kuhakikisha watoto wetu wanaondokana na tatizo hili.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa Daktari Hamza aliyesimama akiafafanua naman ya utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi katika uzinduzi wa chanjo hiyo
Kwa taarifa zaidi pakua nyaraka hii hapa chini:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.