(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi akiwa na Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja pamoja na baadhi ya wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo amefanya ziara katika miradi sita yenye thamani ya Tshs.1,599,800,000.00. katika miradi hiyo, miradi mitatu ni ya sekta ya Elimu ambayo ni Shule ya Sekondari Pwaga imepata fedha Tsh. 66,600,000.00, Shule ya Sekondari Massa imepata fedha Tsh. 66,600.000.00 na Shule ya Sekondari Chipogoro imepata Tsh. 66,600,000.00, Miradi mingine Mitatu ni ya sekta ya Afya ambayo ni Kituo cha Afya Pwaga imepata fedha Tsh. 500,000,000.00, kituo cha Afya Kibakwe imepata fedha Tsh. 400,000,000.00 na Kituo cha Afya Mima imepata fedha Tsh. 500,000,000.00. Fedha zote za ujenzi wa vituo vya afya ni fedha serikalini katika Mfuko Maalum wa Afya. Kwa ujumla vituo vyote vitatu vya afya vipo katika hatua ya umaliziaji.
Kwa upande wa sekta ya Elimu shule ya Sekondari Pwaga ilipewa fedha kiasi cha Tsh 66,600,000.00 zilizotolewa toka Mradi wa Lipa kutokana na Matokeo (P4R) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3 na matundu ya vyoo 6 ambapo ujenzi umekamilika na madarasa na vyoo vinatumika. Katika fedha hiyo iliyotolewa, ni Tsh 56,615,500.00 na fedha iliyobaki Tsh 9,984,500 iliombewa idhini ili itumike katika ukarabati wa jengo utawala, ununuzi waviti 30 vya walimu, kuweka umeme katika nyumba za walimu, kukarabati vyoo vya zamani vya wanafunzi, kununua meza za walimu na kukarabati madarasa 10 ya zamani.
Mhe. Nghwenzi amempongeza sana mkuu wa shule ya sekondari Pwaga kwa usimamizi mzuri wa fedha na miradi ya serikali na kwa kununua vifaa vya ujenzi kwa bei ya soko (bei halisi). Pia ametoa wito kwa wataalam wote wa Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa kusimamia miradi ya serikali vizuri na kwa ubora kama Mkuu wa Shule ya Sekondari Pwaga Ndug. Augustine Senya.
Mojapo ya darasa la shule ya sekondari Pwaga lilojengwa kwa fedha za P4R, jumla ni madarasa matatu yamekarabitiwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi (wanne kushoto) akiwa katika moja ya darasa lililojengwa kwa fedha za P4R akionyeshwa madawati na kukagua ujenzi uliofanyika.
Jengo la Choo cha matundu sita kilichojengwa kwa fedha za P4R katika shule ya sekondari ya Pwaga
Kwa upande wa sekta ya Afya, Kituo cha Afya Kibakwe kimepokea fedha Tsh 400,000,000.00 toka serikalini katika Mfumo Maalaum Wa Afya ambapo fedha hizo zimetumika kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ndani yake kuna maabara na ofisi mbalimbali za madaktari, chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi, wodi ya wanaume, wodi ya wanawake, nyumba ya mtumishi na jengo la kuhifadhia maiti. Mpaka sasa Majengo yote yapo katika hatu ya umaliziaji na matengenezo madogo madogo na ifikapo Novemba 30, 2018 kituo hiki cha Afya kitakuwa kimekamlika na kuanza kutumika.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi amemuagiza mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye ni Afisa utumishi na rasilimali watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa asimamie ukamilishwaji wa Kituo hiki cha Afya na ifikapo tarehe 30 Novemba 2018 wananchi waweze kupata huduma iliyokusudiwa. Pia ameagiza kuwa ifikapo tarehe 30 Novemba 2018 vituo vyote vitatu maana Kituo cha Afya Mima, Kituo cha Afya Kibakwe, na Kituo cha Afya Pwaga viwe vimekamilika ili wananchi wapate huduma.
Jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Kibakwe
Jengo la Wodi ya Akina Mama Kwa Ndani katika Kituo cha Afya Kibakwe
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi (katikati) akielekea kwenye jengo la kuhifadhia Maiti katika Kituo cha Afya Kibakwe.Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) Kituo cha Afya Kibakwe
Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.