Kamati ay Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) leo imetembelea miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Miradi hiyo ni Ujenzi wa Nyumba ya walimu Shule ya Msingi Lukole kata ya kingiti, Ujenzi wa Bwaro na Ofisi ya Walimu Katika Shule ya Sekondari Kibakwe kata ya Kibakwe, Ujenzi wa Kituo cha Afya Chipogoro kata ya Chipogoro na Kituo cha Afya Mtera kata ya Mtera. Katika ziara hiyo ya ukaguiz wa miradi imeongzwa na Mkamu Mwenyekiti wa Halmashaur ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini akiambatana na Wajumbe wa kamati ya Fedha. Pia ziara hiyo imeabatana na Timu ya Wataalam iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Mamba Sweya.
Miradi ifuatayo imetembelewa:-
1. Ujenzi wa Nyumba za Walimu katika Shule ya Msingi Lukole.
Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya walimu mbili katika eneo moja (two in one) yenye jumla ya vyumba sita inayoendelea kujengwa ambapo imefika katika hatua ya kupaka rangi, kuweka madirisha ya vioo na kumalizia ujenzi wa choo. Jengo hili limegharimu kiasi cha Shilingi Milioni thelathini na tano na laki tano (Tsh. 35,500,000/=) hadi kukamilika, kwa mchnganuo ufuatao:- Serikali Kuu Ofiis ya Rais TAMISEMI imetoa Ths 25,000,000/= baada ya kuandika andiko, nguvu za wananchi wamechangia Ths 8,500,000/= na Mhe. George Simbachawene Mbunge wa Jimbo la Kibakwe amechangia Tsh 2,000,000/= kupitia Mfuko wa Jimbo. Jengo hilo linatarajiwa kumalizika tarehe 29/05/2020.
Aidha, baada ya kukagua jengo hilo kamati ya Fedha imegundua mapungufu na kuagiza kuwa Rangi ya kijani iliyopakwa kwa ndani ibadilishwe na ipakwe rangi ya klim (creem), mbao ya fidherboard moja imepinda iondolewe, Mkurugenzi afanye tathimini na kuongeza fedha ili kukamilisha ujenzi wa jengo hili. Kamati ya FUM imepongeza ujenzi mzuri wa mradi huu na kusema kuwa mafundi hao wapewe vyeti kwa ujenzi wao mahiri na kujitoa kwa moyo mmoja kufanyakazi hii.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime (katikati) Akiuwa na Kamati ya FUM katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Nyumba mbili kwa moja kwenye Shule ya Msingi Lukole.
2. Ujenzi wa Bwaro na Nyumba ya Ofisi ya Walimu katika Shule ya Sekondari Kibakwe.
UJenzi wa Bwaro umegharimu Shilingi milioni mia moja, toka Serikali Kuu ambapo jengo limekamilika bado umaliziaji wa choo, jiko na milango. Hata hivyo fedha yote iliyoletwa imeisha ila hakuna
fundi wala mtu yeyote anayedai fedha katika ujenzi wa jengo hili. amesema Sajigwa Nikupala, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibakwe. Pia jengo la Ofisi ya Walimu iligharimu shilingi Milioni tano tu, na kwa sasa jengo hilo linatumika. Aidha, kamati ya FUM baaada ya kukagua na kusomewa taarifa ya majengo hayo imepongeza ujenzi unaoenda na na dhamani ya fedha. Pia Mhe. Fuime ameagiza kuwa katika jengo la
Bwaro wananchi wa kibakwe wahamasihswe ili kuweza kuchangia nguvu zao ili kukamilisha ujenzi huu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime (kulia) Akiuwa na Kamati ya FUM katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Bwaro kwenye Shule ya Sekondari Kibakwe
3. Jengo la Kituo cha Afya cha Chipogoro.
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imepata fursa ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Chipogoro chenye jengo moja tu la wagonjwa wa nje (OPD) kitakachogharimu shilingi milioni mia mbili mpaka kukamilika. Fedha hizo zimetoka Serikali Kuu.
Kwa sasa jengo hilo limefika hatua ya lenta na ujenzi unaendelea na fedha iliyotumika ni shilingi milioni arobaini na tano kama ilivyosomwa katika taarifa ya ujenzi huo. FUM imepongeza jinsi mafundi walivyo na kasi ya ujenzi, wananchi kujitolea eneo na kuleta mchanga na mawe kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Baada ya Kugagua Kamati ilibaini matofali mabovu na kuagiza matofali hayo yasitumika na yaondolewe katika eneo hilo mara moja. Pia Mhe. Fuime ameagiza kuwa eneo lote la mradi lipimwe na liwekwe alama za mipaka (becons). Vile vile amesema kuwa ukuta wa jengo linatakiwa kumwagiliwa mara tatu kwa siku ili liweza kuwa imara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime (wa kwanza mbele) Akiuwa na Kamati ya FUM katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Chipogoro.
4. Ujenzi wa Kituo cha Afya Mtera:
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango mwisho imetembelea mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Mtera chenye majengo ya Maabara, Jengo la Mihonzi, upasuaji, wodi ya wazazi, na chumba cha kuhifadhi maiti. Kituo hiki kitagharimu shilingi milioni mia nne mpaka kukamilika na fedha hizo zimetoka Serikali Kuu. Kwa sasa majengo yote yapo katika hatua ya msingi na ujenzi unaendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime Akiuwa na Kamati ya FUM katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Mtera.
FUM imepongeza jinsi mafundi walivyo na kasi ya ujenzi, wananchi kujitolea eneo na kuleta mchanga na mawe kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. Pia FUM imeagizwa kuwa gari aina ya lori la kubeba mchanga na kokoto lisiloweza kumwaga lenyewe kwa sababu ya ubovu wa hydrolic litengenezwe ili liwezi kufanyakazi hiyo.
Mwisho Mhe. Fuime amewataka Waheshimiwa madiwani kwa kushirikiana na Watendaji wa kata katika kata zao waweza kuwahamasisha wananchi kujitlea katika kuchangia nguvu kazi katika maendeleo ya ujenzi wa miradi hii kwa kuwa manufaa ya miradi hii ni ya wananchi wa kata husika.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.