Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango(FUM) imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Mpwapwa Aprili 29,2025.
Wakati wa ziara hiyo kamati imetembelea ujenzi wa Jengo la Maabara ya kisasa katika kituo cha Afya Kibakwe lililofadhiliwa na Shirika la KOFIH,mradi huo utatagharimu kiasi cha Sh.94,000,000.
Pia wametembelea mradi wa ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya kwa kupokea kiasi cha shilingi 67,000,000 kutoka kwa wafadhili wa Shirika la KOFIH kwa ajili ya manunuzi ya genereta pamoja na vifaa vya umeme pamoja na ujenzi wa genereta shed.
Halikadhalika wametembeleaa Shule ya Sekondari Sijila iliyopo Pwaga kwa ajili ya kujionea maendelea ya kumalizia ujenzi wa shule hiyo iliyogharimu kiasi cha shiling 544,225,626 kutoka SEQUIP.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.