Mkoa wa Dodoma umefanya mkutano wa wadau wa Elimu Machi 25,2024 ikiwa ni kilele cha juma la wadau wa Elimu lililozinduliwa rasmi Machi 19,mkutano huo umehudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Mjaaliwa kwenye Ukumbi wa TAG Mipango,jijini Dodoma.
Lengo la Mkutano huo ni kujadili namna ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Mkoa wa Dodoma pamoja na kuweka mikakati ya kuinua Taaluma na ufaulu kimkoa.Waziri Mkuu ameipongeza Dodoma kwa kuandaa mkutano kwani unakwenda sambamba na Sera ya Elimu ya Nchi.Kauli mbiu ya mkutano huo inakwenda sambamba na sera ya Elimu ya nchi inayosisitiza Uwajibikaji.utoaji wa Elimu bora ni vipao mbele vya nchi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,aesema Serikali yaawamu ya sita imefanya mambo mengi kwenye sekta ya Elimu.
"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuinua sekta ya Elimu Dooma kwani tumeimaika sana miaka mitatu hii.Dodoma imepanda ufaulu wa darasa la 7 na kuingia kumi bora kitaifa 2022 kwa ufaulu kupanda kutoka 83%(2022)hadi87%(2023).Tumeanza kuweka mikakati ya Mkoa kuhakikisha kila mwaka ufaulu unapanda.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.