Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani , Kitaifa imeadhimishwa Mkoani Dodoma, huku Mgeni Rasmi Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza mamia ya Wakunga ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuwaheshimu Wakunga kwakuwa ni watu muhimu katika jamii. Amesema kuwa Wakunga ni mama zetu na ndio watu wa kwanza kutuona pindi tulipoingia hapa Duniani. Kutokana na Umuhimu wao na changamoto za Makazi wanazozipata amezitaka Halmashauri zote Nchini kujenga Nyumba za Watumishi katika Vituo vya Kutolea huduma huku kipaumbele wakipewa Wakunga kwakuwa asilimia kubwa ya wagonjwa wanaokwenda katika vituo hivyo ni akina mama Wajawazito. Vile vile amewaasa Wakunga kufanya kazi kwa weledi na ufanisi.
Viongozi Mbali mbali wa mkoa wa Dodoma wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, Leo Tarehe 05.05.2017 .Wa Kwanza Kutoka Kushoto ni Mhe Jabir Shekimweri Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.
Wakunga wakiwa na Nyuso za Bashasha wakiadhimisha Siku Yao, Leo Tarehe 05.05.2017
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.