Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H.Ally amefanya ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo ya kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Ziara hiyo iliyofanyika Octoba 21,2025 akiambatana na wakuu wa idara na vitengo ametembelea kata ya Kimaghai,Mazae na Mpwapwa Mjini.
Katika kata ya Kimaghai ametembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Inzovu ambayo imegharimu kiasi cha shilingi 60,170,00 kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa P4R kwa ajili ujenzi wa mnara wa tank la maji na ununuzi wa lita 10,000,kitakasa mikono,kichomea taka,shimo la kondo la nyuma la mama baada ya kujifungua,choo cha watumishi na choo cha wateja pamoja na kufanya maboresho ya chumba cha kujifungua,Mradi umekamilika kwa asilimia 100.
Hata hivyo ujenzi wa Zahanati ya kimaghai ambayo imepatiwa kiasi cha fedha 60,000,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya umaliziaji wa Zahanati hiyo na vyoo,ujenzi unaendelea.
Kwa upande wa Mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Msejelele ambayo imepatiwa shilingi 78,165,00 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo,ujenzi unaendelea na umefikia hatua ya upauaji.
Halikadhalika ametembelea ujenzi wa mradi wa Zahati ya Iyoma iliopo kata ya Gulwe ambayo imepatiwa kiasi cha shiling 60,000,000 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la zahanati lililoanzishwa na nguvu za wananchi,ujenzi unaendelea na upo katika hatua ya upigaji lipu jengo,na kiasi cha shiling 30,000,000 kimeshatumika.
Pia amekagua ujenzi wa Nyumba za wakuu wa idara ambazo zimepatiwa kias cha shilingi 350,000,000 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya umaliziaji wa nyumba hizo,hatua iliyofikia ni muendelezo wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuendelea n ujenzi huo.
Ziara hiyo ilimalizia ukaguzi wa ujenzi wa Ofisi mpya ya Halamshauri inayoendelea kujengwa Mbuyuni iliopo kata ya Mpwapwa Mjini,ambayo kiasi cha shilingi 800,000,000 fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo kwa hatua ya mwanzo,kazi bado inaendelea.
Mkurugenzi Mtendaji amewata wasimamizi wa miradi hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi wao ili kuendana na muda uliopangwa na pia kuengeza nguvu kazi









Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.