Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh Dkt Sophia M Kizigo ameshiriki pamoja na Wananchi wa kata ya Gulwe na Berege kusherehekea Siku ya Samia Day iliyoandaliwa na Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuonesha Mafanikio mbali mbali kwa Wananchi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wilaya zake yaliyopatika kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Dkt Samia Suluhu Hassan.
Wakati wa Hafla hiyo Wanachi waliadhimisha kwa michezo tofauti ikiwemo mpira wa miguu na ngoma za asili.
Mh Kizigo amechukua fursa hiyo kuelezea vitu vilivyofanikiwa kufanyika kwa kipindi cha miaka minne tu ya uongozi wa mama Samia ikiwemo miradi mikubwa iliyonagharama lukuki.
Sherehe hizi zilifanyika June 03,2025 katika kijiji cha Gulwe kwa kata ya Gulwe na Mzase katika kata ya Berege.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.