Januari 06,2025 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Dkt Sophia M Kizigo amefanya ziara ya kukagua na kupitia Miradi mbali mbali ya kimaendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2025.
Katika ziara yake hiyo amekagua Jengo la karakana la kuhifadhia dhana za kilimo liliopo Ng'ambi ambalo limegharimu kiasi cha Tsh 55,623,000 pamoja na kukuagua Kichomea taka,mnara wa kuekea tanki la maji na vyoo vya watumishi katika kituo cha Afya Ng'ambi.
Pia ametembelea ujenzi wa Daraja la Kikombo roud ambalo ujenzi wake utagharimu Tsh 300,000,000 na kisha kutembelea kikundi cha vijana na Mshikamo kilichokuwepo Mpwapwa Mjini ambacho kinachojishuhulisha na kuuza bidhaa za mitumba mikoba pamoja na viatu na kimebahatika kupata Mkopo wa asilimiaq 10% Tsh 8,000,000.
Halikadhalika amekagua Mradi wa Maji uliopo kijiji cha Mgoma kata ya Godegode na Kumalizia na Shule ya Sekondari Simbachawene ya kata ya luhundwa iligharimu Tsh 544,225,626.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.