Tunamshukuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kutuengezea kiasi cha Shilingi Billion Moja kwa kumalizia Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri ili kuweza kutatua changamoto za Watumishi kutumia jengo lisilokidhi mahitaji yao.
Awali Halmashauri ilipokea kiasi cha Shilingi Milion 800 kwa hatua za mwanzo za ujenzi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Dkt Sophia Mfaume kizigo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary S Senyamule wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya kimaendele inayoendelewa kujengwa katika Halmashaùri hiyo iliyofanyika Septemba 18,2025.
"Tunamshukuru Mhe Rais kwa kutuengezea Shilingi Billioni Moja kwa ajili ya kumalizia jengo la Ofisi ili Wananchi kero na changamoto zao zishuhulikiwe na kurudisha huduma karibu na Wananchi"amesema Dkt Kizigo
Mradi mwengine uliotembelewa ni ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Afya 3 in 1 na ununuzi wa vifaa tiba katika kituo cha Afya Mima unaofadhiliwa na Shirika la KOFIH 2024/2025 na kugharimu kiasi cha Milion 110,mradi huu una lenga kusaidia makaazi ya watumishi wa kituo hicho wapatao watao na umefikia 89% za utekelezwaji wake.
Halikadhalika,umetembelewa Ujenzi wa mradi wa Ofisi ya Afisa Tarafa wa Mima ambao utagharimu kiasi cha Shilingi 152,ukiwa na lengo la kurahisisha huduma kwa Wananchi na kutatua changamoto zao,mradi umefikia 84% za utekelezaji wake na kuelezwa kuwa jengo ambalo lilokuwa linatumika awali limejengwa 1956.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepokea imepokea jumla ya fedha kiasi cha Shilingi Billion 1.6 kutoka Serikali kuu mwezi Juni 2025 kwa madhumuni ya kuendeleza ujenzi wa ofisi za kutolea huduma za Wananchi na kuzipata kwa karibu.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.