(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo imetoa mafunzo kwa watumishi, wanachuo, wanafunzi wa shule za sekondari na wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa juu ya njia za kutambua fedha halali. Katika mafunzo haya yanamadhumuni ya kuwaabalisha wananchi katika kutambua fedha halali ili wasiweze kutapeliwa kirahisi kwa kupewa fedha bandia. Pia imeelezwa kuwa fedha bandia husababisa kudumaza uchumi wa mwanachi mmoja mmoja pamoja na Taifa kwa ujumla, zinasababisha watu kutofaka kazi au biashara kwa kuogopa kulipwa fedha bandia.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Sarah Komba (aliyesimama) akifungua mafunzo yanayoendeshwa na BOT ya kutambua fedha halali katika Ukumbi wa CCM Wilaya
Akifungua mafunzo haya Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Sarah John Komba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wadau wote waliohudhuria kuwa wasikivu na makini katika kufuatilia mafunzo haya kwa kuwa yana umuhimu mkubwa katika jamii zetu. Pia Bi. Komba amesema "naomba muwe makini kwa kuwa
wananchi wengi hawana uelewa wa utambuzi wa noti halali, hivyo ninyi mtakuwa walimu kwa wengine". Mwisho amewakaribisha wawezeshaji toka BOT kuanza kutoa mafunzo.
Mwezeshaji toka BOT akitoa mafunzo ya utambuzi wa fedha halali katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpwapwa
Mwezeshaji toka BOT baada ya kukaribisha, ametoa mafunzo ya kutambua noti halali:-Kuna njia tatu za kutambua noti halali za aina zote za Tanzania (1) Kwa kuangalia noti kwa macho (2) Kwa kupapasa (3) Kwa kutumia vifaa maalum
(1) Kwa kuangalia kwa macho.
- Kuangalia picha mficho ya mwalimu Julius K. Nyerere.
- Katika picha mficho ya mwalimu Julius K. Nyerere katika kidevu kumeandikwa thamani ya noti husika.
- Kuangalia utepe wa mstali unaong'aa kama kioo.
- Juu ya kichwa cha picha mficho ya Mwalimu Nyerere kuna nukta nukta ambazo ukiangalia kwa makini zitaunganika na kufanya tarakimu ya thamani ya fedha.
- Nyuma ya fedha kuna picha ya twiga na inamng'ao kama dhahabu na huwa inabadilika kuwa kijani au bluu.
(2) Kwa kupapasa
- kupapasa pembeni ya noti, huwa kunakuwa kama kuna nundu nundu.
- Chini ya maneno Benki Kuu ya Tanzania kuna maneno madogo yameandikwa fedha halali kwa malipo ya shilingi...... huwa yanakuwa yana nundu nundu.
- chini ya picha mficho ya mwalimu nyerere kuna mistari ya V ukipapasa inakuwa na nundu nundu.
-
(3) Kwa kutumia vifaa maalum (tochi ya mwanga wa bluu)
- Mulika tochi/taa ya mwanga wa bluu katika namba ya fedha, itaakisi mwanga kama reflectors.
- Mulika upande wa picha mficho ya mwalimu Julius K. Nyerere na utaona kiboksi kimeandikwa TZS na thamani ya noti husika.
-Mulika sehemu ya nyuma chini ya twiga utaona maua yanawaka.
Baada ya kufundishwa njia hizo tatu, washiriki waliruhusiwa kufanya utambuzi wa fedha halali kwa vitendo na kubaini fedha walizonazo zilikuwa halali.
Mshiriki Ndug. Baraka Msuya (aliyesimama) akielezea namna ya kutambua fedha halali wakati wa mafunzo ya BOT katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpwapwa
Mwezeshaji ametoa wito kuwa fedha zitunzwe benki na kama kina kiasi kidogo kwa ajili ya matumizi kutunzwe kwenye waleti na sio kuikunja katika pindo za nguo. Mwezeshaji aliomba mshiriki mmoja aelezee jinsi ya kutambua fedha halali ambapo Ndug. Baraka Msuya toka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii alielezea kwa usahihi njia zote tatu za kutambua fedha halali na mafunzo yalifungwa.
Kwa maelezo zaidi soma vipeperushi vya BOT hapa chini
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.