Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Sophia Mfaume Kizigo leo Oktoba 11,2024 amezindua Uwandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa Shamra shamra za mazoezi ya kukimbia kwa pamoja na baadae kupita kituo hadi kituo kujiandikisha pamoja na watumishi wake.
Katika Ufunguzi uwo wa Kibabe wa Daftari la Wapiga kura Mhe. Kizigo amewataka Vijana, wazee, watumishi wa Umma na wa binafsi na wale wote wanaotarajia kufikisha umri wa miaka 18 mpaka ifikapo Novemba 27,2024 waende kujiandikisha mapema na wasisubiri siku ya mwisho ya uwandikishaji.
"Nasisitiza jamani watu wote walio na sifa waende kujiandikisha mapema katika vitongoji vyao wanavyoishi, vijana, wazee, watumishi na wale wote wanaotarajia kufikisha umri wa kupiga kura kabla ya tarehe ya Uchaguzi wakajiandikishe"amesema Dkt Kizigo
Naye Afisa Uchaguzi Wilaya Bw. Thomas Magali amewasisitiza vijana kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la Uwandikishaji wapiga kura na wasisite na jirani zao
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.