Meneja Miradi EcoKazi Advisory Limited Bw.Rutamanyirwa Laurent ametoa mafunzo kwa wakuu wa Idara na vitengo pamoja na baadhi ya watendaji wa vijiji yanayohusiana na biashara ya Carbon Julai 22,2025 katika Ukumbi wa Baishara wilayani Mpwapwa.
Wakati wa mafunzo hayo Bw.Laurent amesema kuna vitu vitatu ambavyo vitaangaziwa ndani yake ikiwemo mabadiliko ya tabia ya Nchi,biashara ya Carbon na miongozo na sheria ya biashara hiyo, lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha Wananchi kukubali kuingia ushirikiano na kampuni ya EcoKazi katika kufanya biashara ya carbon ili waweze kujikidhi katika mahitaji yao ya kila siku.
Hata hivyo, ameelezea sababu zilizowasukuma kuanzishwa kwa biasha ya carbon ni pamoja na maendeleo ya viwanda yanayozalisha hewa ya ukaa,kupambana na muhimili wa mabadiliko ya tabia Nchi kupitia vyombo mbalimbali vilivyoundwa pamoja na sera za mazingira,vilevile ameelezea hatua ambazo zinazoweza kupambana na madiliko ya tabia ya Nchi kwa kuundwa vyombo vya carbon kwa miradi endelevu
Mwisho amewashauri wanamafunzo hao kuendelea kutunza mazingira ili uzalishwaji wa carbon uendelee na ipate kutumika kwa watu na pia kujiingizia kipato,biashara ya carbon inalenga namna gani wananchi wataweza kutunza misitu na kuanzisha misitu mipya,biashara ya carbon inaweza kuzalishwa kupitia misitu,kilimo,nishati,ardhi, usafirishaji,usimamizi wa taka na sekta ya viwanda.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.