Afisa Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Muba akiambatana na timu ya Ufuatiliaji wa miradi ya kimaendeleo Mkoa Julai 21,2025 wamefanya ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo wilayani Mpwapwa na kukagua Shule ya Sekondari ya Amali Mpwapwa iliyogharimu kiasi cha Sh 544,225,626.pamoja na jengo la maabara la kituo cha afya Kibakwe ambalo mpka kufikia hatua ya umalizikiaji litagharimu Sh.94,000,000.
Wakati wa ziara hiyo Afisa Tawala Msaidizi na timu yake wametoa maelekezo ya maboresho madogo madogo walivyoyabaini katika.majengo na pia walihimiza mafundi kukimbizana na muda wa kumalizia mradi wa jengo la maabara la kituo cha afya Kibakwe kwani wapo nje ya muda wa mkataba wao.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.