Mradi wa Behavioural Adaptation for Water Security and INclusion (BASIN)umetoa mafunzo kwa viongozi na wataalam kuhusu taarifa za tahadhari ya mapema ili kuweza kukabiliana na majanga ya hali ya hewa kutokana na mabadiliko ya tabianchi Sepptemba 10,2025 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.
Mkurugenzi kutoka Shahidi wa Maji ameieleza BASIN ni mradi wa kiutafiti unaojaribu kuunganisha,kutathmini,na kutumia maarifa kutoka katika Sayansi ya tabia na saikoloji ili kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuengeza uhakika wa maji uliojumuishi kwa makundi yaliyo hatarini zaid.
Hata hivyo,amesema suala la uhakika wa maji ni suala la kimsingi la usalama wa Taifa hii ni kwa sababu bila ya maji uhakika wa chakula,pia ili nishati safi ipatikane katika Nchi ni lazima uhakika wa maji uwepo hii ni kwasababu maji ndio chanzo pekee cha uzalishaji wa umeme.
Halihadhalika amesema Maji ni silaha,ila huathiriwa na vitu tofauti ikiwemo Mabadilko ya tabianchi,tabia za kibinaada zinazopelekea kuharibu vyanzo vya maji.
"Haya maji yanaathiriwa na changamoto tofauti tofouti,changamoto moja wapo ni badiliko ya tabianchi yanaathiri vyanzo vyetu vya maji na tabia za kibinaadam na ndio maana leo tunazungumza habari ya rasilimali maji na mabadiliko ya tabianchi"amesema Bw.Dugange
Nae Meneja huduma za hali ya hewa kwa rasilimali maji Ndg Suleimani Chillo amesema lengo la mradi ni kutoa tahadhari za mapema, na kutoa taarifa ya hali ya hewa kuweza kutumika sawa sawa kwa wakulima na wafugaji ili waweze kujiandaa na hali ya hewa ya baaadae,hii ni kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanyika na kubainika taarifa za hali ya hewa hazifiki kwa wananchi na wala hakuna taarifa mahsusi inayotolewa kutoa tahadhari.
Vilevile ameelezea Mamlaka ya hali ya hewa hutoa taarifa pindi kutakapokuwa na viashiria vya mvua kubwa,ili kuweka tahadhari kwa wananchi kuepukana na madhara ambayo yanaweza kutokea.
Taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hali ya hewa kwa Mpwapwa imewasilishwa ikiambatana na angalizo,uwezekano wa kutokea kwa majanga pamoja na kiwango cha athari zinazoweza kutokea.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.