Baraza la Biashara la Wilaya ya Mpwapwa ambalo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo tarehe 30 April 2018 limefanya kikao chake cha kujadili Mikakati ya kujenga viwanda Wilayani Mpwapwa. Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe wote wa sekta ya umma na binafsi ambao kwa idadi yao walikuwa 46.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini kikao cha Baraza la Biashara Juu ya Mikakati ya Kuanzishwa Viwanda.
Katika Mikakati ya Kujenga viwanda, Baraza hilo limejadili kwa kina aina ya viwanda vinavyotarajiwa kujengwa Wilayani Mpwapwa ni kama ifuatavyo:-
1. Viwanda Vidogo sana (Micro enterprise ) ambvyo vitaajiri wafanyakazi kuanzia mtu 1 hadi 4 na mtaji wake ni hadi kufikia Tsh. milioni 5.
Mfano wa viwanda vidogo sana vinavyotarajiwa kujengwa Mpwapwa (Picha na; SIDO)
2. Viwanda Vidogo (Small Enterprise) ambavyo vitaajiri wafanyakazi kuanzia 5 hadi 49 na mtaji wake ni zaidi ya Tsh. Milioni 5 hadi Milioni 200.
Mfano wa viwanda vidogo vinavyotarajiwa kujengwa Mpwapwa (Picha na: SIDO)
Mfano wa viwanda vidogo vinavyotarajiwa kujengwa Mpwapwa (Picha na: SIDO)
3. Viwanda Vya Kati (Medium Enterprise) ambavyo vitaajiri wafanyakazi kuanzia 50 hadi 99 na mtaji wake ni zaidi ya Tsh milioni 200 hadi Tsh milioni 800.
Mfano wa viwanda vya kati na vikubwa vinavyotarajiwa kujengwa Mpwapwa (Picha na: SIDO)
4.Viwanda vikubwa (Large Enterprise) ambavyo vitaajiri wafanyakazi kuanzia 100 na kuendelea, na mtaji wake ni zaidi ya TSh. Milioni 800.
Aidha katika kikao hicho, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) wamefanya wasilisho la Uanzishwaji na Uendelezaji wa Viwanda kwa Mfumo wa Kongano, ambalo madhumuni makuu la wasilisho hili ni kueleza mikakati na jinsi ya kuanzishwa kwa Viwanda Wilayani Mpwapwa. Pia pia wasilisho hilo limeonyesha shughuli muhimu za kiuchumi katika wilaya ya Mpwapwa ambazo ni Kilimo cha Mazo kama mahindi, karanga, alizeti na Mifugo kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo. Kwa shughuli hizi viwanda tarajiwa vitapata malighafi kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
Baada ya Kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa amepongeza mikakati hiyo ya kuinua uchumi wa wilaya kupitia mapinduzi ya viwanda. Pia ameaidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha mikakati hiyo na ni ndoto yake ya muda mrefu kuona Mpwapwa inapata viwanda na Eneo la Pamoja la Kibiashara (Commercial Hub) ambapo kwa sasa eneo limeshatengwa kwa ajili ya Commercial Hub.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.