Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa linaoongozwa na Mwenyeki wake Mhe. George Fuime limewaarika Meneja wa Shirika la Umeme Tanzani wa Wilaya ya Mpwapwa (TANESCO), Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Meneja wa Mamlaka ya Maji Mijini na Vijijini kuja kutoa ufafanuzi wa utoaji wa huduma hizo kwa wananchi wa wilaya ya Mpwapwa hususani katika Kati zilizopembezoni na makao makuu ya Wilaya.
Akieleza shughuli zilizopangwa kufanyiika katika wilaya ya Mpwapwa kwa Upande wa Usambazaji umeme Meneja wa TANESCO amesema "Kwa sasa Shirika la Umeme linatekeleza miradi ya kumalizia kusambaza nguzo katika baadhi ya maeneo ya vijiji vya Kata ya Vinghawe, Mbuga, Galigali, Malolo, Galigali, Ipera na Lupeta". Vile vile ameongeza kuwa Shirika limefanya tathin na linatarajia kufunga Tranforma na kusambaza nguz za umeme katika Eneo la Mazae lenye mradi wa Viwanja takribani 1,000.
Kwa Upande wake Meneja wa TARURA amesema "Kwa sasa wanafanya ukarabati wa barabara zote zilizoathiriwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha ili shughuli za kiuchumi kwa wananchi ziweze kuendelea. Mvua zikiisha kuanzia mwezi wa May mwaka huu ndio tutafanya matengenezo makubwa na kuchonga barabara mpya mfano barabara ya Mtera kwenye chibwegele na Chugu na zinginezo". Pia TARURA kwa uwezeshaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imeweza kutengeneza barabara za kuzunguka na za ndani katika eneo la mradi wa viwanja 1000 la Mazae.
Meneja wa TARURA Mhandisi Lukuyi akiwasilisha mada ya barabara katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Naye Menejawa RUWASA Wilayaya Mpwapwa amesema kuwa kuna mpango kabambe wakuchimba visima virefu visivyopungua vitatu katika Wilaya ya Mpwapwa hasa kwa hapa mjini ili kupunguza adha ya maji, visima hivyo vitachimbwa Kijiji cha Mazae kata ya Mazae, Isinghu kata ya Vighawe na Lupeta kata ya Lupeta. Kazi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu kwakuwa mashine za uchimbaji kwa sasa zipo Wilaya ya Kongwa zinafanyakazi na baada ya kumaliza huko zitahamia Wilaya ya Mpwapwa.
Meneja wa RUWASA akiwasilisha mada ya hali ya upatikani madi katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.