Baraza la Madiwani limefanyika leo katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambapo agenda mbalimbali zilijadiliwa zinazohusu maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikiwemo maendeleo ya shule na ufaulu mzuri wa matokeo ya darasa la saba katika kumaliza elumu ya msingi, maji, barabara na mapato. Katika agenda ya mapato ilijadiliwa kwa kina kwa kulinganisha mapato ya kila mwezi yanayoletwa na watendaji na mapato yaliyokusanywa na Timu ya Tathmini ya Mapato kwa muda wa siku tatu, ambapo kwa siku tatu Timu ilipatika Tsh 7,902,100/= kata ya Mtera kwa ushuru wa samaki wakati kwa mwezi mtendaji huwa analeta kiasi hicho au chini ya hapo.
Agenda hii ya mapato na hasa taarifa ya Timu ya Tathmini ya Mapato iliwasisimua wageni waalikwa na viongozi wa nchi hususani Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri kwa kuwa mapato yanayokusanywa na watendaji hayana uhalisia. Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Wilaya ameamua kuunda Tume Maalum ya Ukaguzi wa Mapato yenye wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mtaalam wa Mifumo ya Kompyuta na Mashine za Kukusanyia mapato (POS) toka OR - TAMISEMI.
Kazi ya kuchunguza uhalisia wa makusanyo ya mapato ya Halmashauri imeanza tarehe 8/2/2018 hadi leo inaendelea kwa kukagua mifumo ya kompyuta, POS, Vitabu na kuwahoji wakusanya mapato (watendaji wa kata). Kwa sasa Tume hiyo ya Ukaguzi wa Mapato inaendelea na uchunguzi itakapomaliza na kutoa taarifa, tutawajuza.
Wageni waalikwa na wakuu wa idara wakisikiliza majadiliano ya agenda ziizowasilishwa.
Wageni waalikwa, wakuu wa idara na waheshimiwa madiwani wakifuatilia kwa umakiji agenda zinazijadiliwa
Kwa taarifa zaidi pakua hapa chini:
TAARIFA MWENYEKITI - KAMATI YA UCHUMI.pdf
TAARIFA MWENYEKITI - KAMATI YA UKIMWI.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.