Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo tarehe 14 Juni 2018 lafanya kikao cha Robo ya Tatu 2017/2018. Kikao hicho kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani wa kuchaguliwa na wa viti maalam, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri, wageni waalikwa, kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa idara, wananchi, watendaji wa kata, maafisa tarafa.
Agenda zilizowasilishwa ni kufungua kikao, kuthibitisha agenda, kupitia na kuthibitisha muhtasari wa kikao kilichopita cha tarehe 8 Februari 2018, maswali ya papo kwa papo, taarifa ya kutoka kwa mkurugenzi mtendaji, taarifa kutoka kwa wenyeviti wa kamati za kudumu: (a) Kamati ya huduma za jamii, (b) Kmati ya Huduma za Uchumi (c) Kamati ya Kuthibiti UKIMWI na (d) Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango. Agenda zingine ni taarifa ya mwenyekiti, salamu toka serikali kuu na kufunga kikao.
Waheshimiwa madiwani wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu 2017/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (Picha. Na. Shaibu J. Masasi -Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Katika taarifa za wenyeviti wa kamati za kudumu, maazimio mbalimbali yameazimiwa na kuwasilishwa mbele ya baraza kwa utekelezaji. Maazimia hayo ni kama yafuatayo:-
Kamti ya Huduma za Jamii: Kamati hii iinaundwa n a jumla ya Idara tano ambazo ni Afya, Maji, Elimu Msingi, Elimu Sekondari na MAendeleo ya Jamii na Vijana. Kamati hii ilifanya kikao chake cha kawaida cha robo ya tatu mnamo tarehe 29 Mei 2018. Mwenyekiti wa kamati ni Mhe. Joctan Cheliga, diwani wa kata ya Lumuma.
Kamati ilijadili taarifa za utekelezaji wa kila idara inayounda kamati hii. Baada ya majadiliano kamati imeshauri na kuazimia yafuatao:-
Kamti ya Huduma za Uchumi: Kamati ya hii inaundwa na idara tano nazo ni idara ya mifugo na uvuvi, idara ya kilimo, umwagiliaji na ushirika, idara ya ujenzi, idara ya ardhi na idara ya usafi na mazingira. Mwenyekiti wa Kati hii ni Mhe. Richard E. Maponda diwani wa kata ya Luhundwa.
Kamati hii ya uchumi ilikaa kikao chake cha kawaida mnamo tarehe 29 Mei 2018 na kuazimia yafuatayo:
Baadhi ya wageni waalikwai wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu 2017/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (Picha. Na. Shaibu J. Masasi -Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Kamti ya Huduma za Kuthibiti UKIMWI: Kamati ya hii inaundwa na idara mbili nazo ni idara ya Afya na idara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto. Mwenyekiti wa kamati hii ni Mhe. George O. Fume ambaye ni diwani wa kata ya Mpwapwa Mjini.
Kamati hii ya ilikaa kikao chake cha kawaida mnamo tarehe 29 Mei 2018 na kuazimia yafuatayo:
Daktari Said Mawji (aliyesimama mbele) ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya akisubiri kukabidhiwa zawadi maalum toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri. Zawadi hiyo imeandaliwa na waheshimiwa madiwani baada ya kuridhishwa na kufurahishwa na utendaji kazi wa daktari hiyo. Zawadi hiyo imetolewa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu 2017/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (Picha. Na. Shaibu J. Masasi -Afisa TEHAMA Mpwapwa)
Kamti ya Huduma Fedha, Uongozi na Mipango: Kamati ya hii inaundwa na idara fedha na biashara, mipango na takwimu, kitengo cha sheria, ukaguzi wa ndani nakitengo cha manunuzi. Mwenyekiti wa kamati hii ni Mhe. Donati S. Nghwenzi ambaye ni diwani wa kata ya Massa.
Kamati hii ya uchumi ilikaa vikao vitatu tarehe 1 Machi 2018, 26 Machi 2018, 9 Juni 2018, na kuazimia yafuatayo:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.