Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kupitia Afisa Muandikishaji Bw..Dismas Pesambili imefanya mafunzo kwa watendaji ngazi ya kata kuhusu mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili, mei 14 2025 katika Ukumbi wa Liti Kikombo.
Katika uzinduzi huo Bw. Dismas Pesambili amewasihi wanufaika wa mafunzo hayo kutumia vizuri elimu watakayopata kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii,weledi,na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili la kitaifa.
Pamoja na hayo amesisitiza kuwa mawakala wa vyama vya siasa wanaruhusiwa kuwepo katika vituo vya uandikishaji lakini hawapaswi kuingilia majukumu ya maafisa waandikishaji.
“Mawakala wa vyama vya siasa wanaruhusiwa kuwepo katika vituo vya wapiga kura jambo hili ni muhimu kwa kuwa linalenga luleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watatumika kutambua wapiga kura wa eneo husika ili kupunguza vurugu zisizo na lazima,mawakala hao hawatakiwi kuingilia majukumu yenu wakati wote wa uandikishaji”
Ikumbukwe kuwa zoezi hili litaanza rasmi kuanzia tarehe 16 mei 2025 hadi tarehe 22 mei 2025.
“Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa taifa bora”
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.