(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mhe. Elirehema Kaaya leo ametembelea miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikiwemo miradi ya Kilimo, biashara na Ufugaji. Haya yamesemwa na katibu mkuu huyo katika Kikao cha kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Mhe. Kaaya amewaambia wajumbe wa Kamati ya Fedha kuwa "Nimeona bora nije kutembelea miradi inayotekelezwa na ALAT katika uhalisia wake baadala ya kukaa ofisini na kupata taarifa tu".
Pia Mhe. Kaaya ametumia fursa hii ya kuongea na wajumbe wa kamati ya Fedha ambao pia ni madiwani katika kata mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa wahamasishe wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura litakalotumika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019.
Waheshimiwa madiwani na wakuu wa idara wakifuatilia kwa makini ujumbe wa Katibu Mkuu wa ALAT
Mhe. Kaaya ameongeza kuwa "nimepata taarifa toka kwa Mkurugenzi Mtendaji kuwa kuna changamoto katika uandikishaji hasa katika maeneo ya vijijini hayafikiki kwa urahisi, wito wangu kuwa maafisa waandikishaji wakaweke kambi huko ili kuhakikisha zoezi hili halikwami".
Mwisho amewashukuru wajumbe wa kamati ya Fedha kwa kukatisha kikao chao muhimu na kusikiliza ujumbe wake, hivyo ametoa taarifa kuwa yupo katika zoezi maalum la ufuatiliaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na ALAT katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.