Wakuu wa Shule za Msingi Mkoa wa Dodoma wametakiwa kuweka utaratibu kwa wanafunzi kukimbia mchaka mchaka asubuhi kabla ya kuana masomo kwanizoezi lina faida nyingi ikiwemo kuimarisha afya ya akili,ukakamavu pamoja na Uzalendo kupitia nyimbo zinazoimbwa wakati wa zoezi hilo.
Hayo yamebainishwa Marchi 19,2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati wa uzinduzi wa juma la wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma iliopo Jijini humo.
Kadhalika,Mkuu wa Mkoa ameungumzia umuhimu wa michezo kwani juma hili linaenda sambamba na Bonanza la Michezo mbalimbali kuelekea kilele chake Machi 24,2024.
"Shirikisho la michezo Tanzania TFF limetoa mipira 1,000 ambayo nitaigawa leo kwenye Halmasauri zote za Mkoa wa Dodoma.Tutafatilia kuhakikisha mipira inatumika na sio kuweka kabatini,michezo ni afya kwani asilimia 30 ya wananchi wanakabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza kutokana na kukosa kushiriki michezo."Amesema Mhe.Senyamule
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.