Kikao cha kamati ya Lishe robo ya April_Juni kimefanyika leo Agosti 8,2024 katika Ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.
Katika kikao hicho taarifa za utekelezaji wa viashiria vya makataba wa Lishe zimepitiwa kwa kipindi cha robo iliyopita ya mwezi Juni 2024 kwa Idara ya Lishe na Elimu.
Pia Afisa Lishe Wilaya Ndg.Eliwaza Ndau alielezea viashiria vinavyopimwa kulinganisha na ukubwa wake pamoja na utekelezaji wa viashiria hivyo,kikiwemo kiashiria cha matumizi ya fedha za watoto chini ya umri wa miaka mitano,kiashiria cha watoto waliopata matone chini ya umri wa miaka miatano,kiashiria cha kina mama wenye watoto chini ya umri wa miaka mitanao waliopata elimu ya lishe na viashiria vyenginevyo.
Halikadhalika ameelezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi cha robo ya tatu ikiwemo engozeko la fedha kwa kila mtoto ukilinganisha na kipindi kiliichopita,ulinzi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma za afya,kutoa matibabu ya watoto wenya utapia mlo mkali,kutoa mafunzo kwa watoa huduma zalishe,kuanzisha mradi mpya wa kilimo na mbogamboga katika Shule ya Sekondari Kimaghai A,upatikanaji wa chakula Mashuleni pamoja na mafanikio ya mchakato wa hatua za awali za kuengeza Mashine za kurutubisha unga wa ugali ili kila Tarafa iwe na mashine yake
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.