UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya sheria ya Biashara Na.25 ya Mwaka 1972 na Marekebisho yake yaliyofanyika june 2014 pamoja na marekebisho katika sheria ya Fedha Na.2 ya Mwaka 2014 na Na.16 ya Mwaka 2015. Mwombaji wa leseni ya biashara anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN211 (Business application form).
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane(18) Mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara kisheria.
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinacho mruhusu kufanya biashara nchini kutoka idara ya uhamiaji.
LESENI ZA BIASHARA ZIMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAWILI:
KUNDI A;Leseni hizi hotelewa na Wizara ya Viwanda ,Bishara na Uwekezaji.(Fomu ya maombi iwasilishwe na Halmashauri kabla ya kupelekwa Wizarani)
Mfano;
KUNDI B:Hizi hutolewa na Halmashauri za Wilaya,Manispaa,Miji na Majiji husika.
Mfano:
UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Kila Mfanyabiashara anatakiwa afike ofisi ya Biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya kuchukua fomu na kujaza kama utakavyoelekezwa .Baadhi ya nyaraka zinazohitajika kama kiambatanisho na masharti katika fomu ya maombi (TFN221) ni ;
MALIPO:Kutokana na marekebisho ya sheria ya fedha Na 2 ya mwaka 2014 ada za leseni hulipwa kulingana na aina ya biashara kama ilivyoanishwa katika jedwali la viwango vya ada kwa mwaka
MUDA WA LESENI: Umri wa leseni ni miezi 12 toka siku ya kutolewa.
MASHARTI YA UTUMIAJI WA LESENI
1.Mwenye leseni hataweka masharti yeyote kwa mnunuzi
2. Mwenye leseni atatoa risiti kwa mauzo yote.
3.Mwenye leseni atafuata sheria ya leseni ya biashara No. 25 ya 1972
4.Mwenye leseni hatatoa huduma/bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora,uliowekwa na Vyombo vinavyotumika kisheria
5.Mwenye leseni anaweza kunyang’anywa wakati wowote ikiwa inaonekana aliipata kwa njia ya udanganyifu au amekiuka masharti ya leseni.
MAKOSA
1.Kuendesha biashara bila leseni
2.Kuendesha biashara eneo tofauti na linaloonyeshwa kwenye Leseni.
3.Kutumia leseni moja kufanya biashara zaidi ya moja au maeneo mawili au zaidi
4.Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara inapotakiwa kufanya hivyo na Afisa aliyedhinishwa na Serikali.
5.Kutokuweka leseni ya biashara mahali ambapo inaonekana kwa urahisi (Kuficha leseni).
6.Kutoa maelezo ya uongo ili kupata leseni au kukwepa kulipa ada /kodi inayostahili
7.Kumzuia Afisa wa Serikali aliyepewa mamlaka ya kukagua kufanya kazi yake.
ADHABU; (i). Mtu yeyote anayetenda mojawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tsh 50,000/= na isiyozidi Tsh 100,000/= au kifungo kisichozidi miaka miwili(2) au faini na kifungo kwa pamoja.
(ii). Mtu yeyote atakayechelewa kuhuisha leseni yake baada ya siku 21 baada ya muda wa leseni kuisha atalipia asilimia 25 ya ada iliyotakiwa kulipia na itaongezeka asilimia 2 kila mwezi kadri mfanyabiashara anavyochelewa kuhuisha leseni ya biashara
NB.Wafanyabiashara wote wanaaswa kufuata na kutekeleza sheria bila shuruti,kwani kutofanya hivyo kunawaingiza gharama zisizo za lazima kama faini na kupoteza muda hasa pale wanapokutwa na makosa
Pakua Fomu ya Maombi ya Leseni Hapa Chini
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.