Friday 10th, January 2025
@
Wakuu wa Idara na Vitengo wapatiwa Semina Elekezi Wilayani Mpwapwa leo tarehe 10/07/2017.
Semina hii elekezi juu wa Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa ajira mpya ili kufahamu taratibu za kazi, sheria, kanuni, namna ya kutoa taarifa katika mamlaka husika. Aidha semina hiyo ilijikita katika kuwawezesha wakuu wa idara na vitengo katika kuwafahamisha wafanyakazi wa ajira mpya juu ya majukumu yao, kazi zao za kila siku, haki zao, na mahali pa kuanzia kutoa taarifa kama watapata changamoto wanapokuwa katika vituo vya kazi. Vilevile wawezeshaji walitoa maswali ambapo washiriki waliyajibu kwa kujadiliana katika makundi matano na kila kundi lilikuwa na washiriki saba.
Mafunzo hayo yalitolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini semina elekezi inayotolewa na wawezeshaji.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini semina elekezi inayotolewa na wawezeshaji.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini semina elekezi inayotolewa na wawezeshaji.
Kwa kufuatilia zaidi Semina Hii Pakua nyaraka hizi hapa chini:
Kiongozi cha Utaratibu wa mafunzo ya awali kwa watumishi wa Umma..pptx
Kiongozi cha Mafunzo ya Awali kwa Watumishi wa MSM - Final - 24th May 2017.pdf
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.