Tuesday 21st, January 2025
@UKUMBI WA HALMASHAURI
Baraza la Madiwani robo ya pili limefanyika leo Machi 3,2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,wakati wa baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.George Fuime amewataka madiwani kuendelea kukusanya mapato hususani kwenye upande wa Madini.
Pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuthibiti mapato kwa kuweka mikakati itakayo tumika kukusanya mapato hayo,vilevile amewasisitiza Madiwani kusimamia ipasavyo miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika maeneo yao.
Nae kaimu Mkuu wa Wilaya Ndg.Obert Mwaliego ametoa maagizo ya maandalizi ya mbio za Mwenge unaotarajiwa kuupokea mwezi wa 6 ukitokea mkoani Iringa,halikadhalika amesisitiza suala la usafi wa mazingira pamoja na Elimu.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.