Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa anatawangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na Kliniki Tembezi ya madaktari bingwa itakayofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kuanzia tarehe 21/10/2018 hdi tarehe 25/10/2018. Kutakuwa na madaktari wa magonjwa ya watoto, Magonjwa ya akina mama na uzazi, Magonjwa ya kinywa na meno, Magonjwa yasiyo ya kuambikiza, Magonjwa ya Macho, Magonjwa ya wanaume na njia ya mkojo, Magonjwa mchanganyiko na upasuaj, Magonjwa ya Mifupa.
Pia kutakuwa na upimaji wa Afya, Uvhunguzi wa Kifua kikuu, Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi, Zoezi muhimu la uchangiaji damu litakuwepo.
Vipimo vyote maalaum vitapatikana katika zoezi hili,
Kumbuka! Huduma hii sio bure bali ni nafuu sana, gharama ya kumuona daktari bingwa ni Tsh. 5,000/- na kwa wenye Bima ya Taifa yaani NHIF au CHF iliyoboreshwa waje na kadi zao zilizo hai gharama zote za upasuaji ni Tsh. 30,000 tu, gharama za vipimo, kitanda na dawa zitalipwa kulingana na aina ya ugonjwa.
MUHIMU: Zoezi zima la Uandikishaji liataanzia Dirisha la Kujiandikisha (Mapokezi), Kuwenda kumuona daktari, Maabara mpaka kununua Dawa litafanyika kwa Kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Kuratibu Matibabu ya Wagonjwa (GoT-HOMIS). Utapatiwa risiti za Kielektroniki zinazotoka katika Mfumo huu kwa malipo halali utakayoyalipa.
WOTE MNAKARIBISHWA, ASANTENI SANA
Kusikia tangazo hili bofya hapa
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.