Kata ya Chipogoro ni miongoni mwa Kata 18 zilizoko katika Jimbo la Kibakwe na ni miongoni mwa Kata 43 zilizofanya uchaguzi mdogo tarehe 26/11/2017 siku ya Jumapili kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa Kata hiyo. Vituo vya kupigia kura katika kata hii vilikuwa 24 ambavyo vilikuwa na jumla ya wapiga kura 5278 waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na ndio waliotarajiwa kupiga kura siku hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji wa uchaguzi mdogo huo utoaji wa fomu kwa ajili ya wagombea ulifanyika kuanzia tarehe 20/10/2017 hadi tarehe 26/10/2017; wagombea watatu kutoka vyama vya CCM, CHADEMA na CUF walichukua fomu za uteuzi. Aidha uteuzi wa wagombea ulifanyika tarehe 26/10/2017 ambapo wagombea wawili kutoka katika vyama viwili vya CCM na CHADEMA walifanikiwa kurudisha fomu hizo na waliteuliwa kugombea nafasi ya udiwani baada ya kukidhi vigezo, ambao ni:
NA |
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
KATA
|
MAELEZO
|
|
M
|
F
|
|||||
1. |
JAFARI JUMANNE SIMBA
|
√
|
|
CHADEMA
|
CHIPOGORO
|
ALITEULIWA
|
2. |
HOSEA MANYIKA FWEDA
|
√
|
|
CCM
|
CHIPOGORO
|
ALITEULIWA
|
Hata hivyo mgombea Udiwani Semeni Yohana Benard kutoka chama cha CUF hakurudisha fomu za uteuzi.
PAKUA HAPA TAARIFA : TAARIFA YA MWENENDO WA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA CHIPOGORO BARAZA LA MADIWANI.docx
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.