Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge anatarajia kufanya ziara kuanzia tarehe 27 Agosti 2018 siku ya Jumatatu hadi 28 Agosti 2018 Jumanne katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Ziara hiyo ni ya kikazi na atambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, kamati ya ulinzi na usalama, baadhi ya waheshimiwa madiwani na wataalamu mbalimbali toka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Siku ya kwanza ya tarehe 27 Agosti 2018 atafanya kikao cha kazi na wtaumishi wote waliopo makao makuu (Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa) na vijijini kwa idara zote katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mpwapwa (TTC) muda ni saa 4 asubuhi. Pia atafanya mkutano wa hadhara huko kata ya Wotta.
ANGALIZO: KWA WATUMISHI WA IDARA YA ELIMU NA AFYA TAFADHALI AJE MTUMISHI MMOJA KUTOKA KILA KITUO ILI HUDUMA ISISIMAME AU KUFUNGWA.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa atatembelea miradi ifuatayo:-
1. Mradi wa Shule ya Sekondari ya Kibakwe.
2. Kituo cha Afya Kibakwe.
3 . Ujenzi wa Maabara Wotta.
4. Ujenzi wa barabara ya Kibakwe - Wotta.
5. Mradi wa Maji katika kijiji cha Mzase.
Wananchi wote mnakaribishwa.
*****Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa***
Kitengo cha TEHAMA
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.