Wananchi wote wa Wilaya ya Mpwapwa Mnatangaziwa kuwa tarehe 16 Juni 2019 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika yatakayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chazungwa. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Mpwapwa Mjini Mhe. George Fuime.
Sherehe hizi zitaambatana na bonanza la mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto wakike na utoaji wa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum. Nyote Mnakaribishwa.